IQNA

Washindi wa Tuzo ya Sayansi ya Mustafa SAW Waenziwa Tehran

22:21 - December 05, 2017
Habari ID: 3471297
TEHRAN (IQNA)-Washindi wa Tuzo ya Kimataifa ya Sayansi ya Mustafa SAW (MSTF) wameenziwa katika sherhe iliyofanyika Jumapili mjini Tehran.

Tuzo hiyo ambayo imetolewa kwa mwaka wa pili sasa inalenga kuwaenzi watafiti Waislamu waliofanikiwa katika nyuga mbali mbali za sayansi na teknolojia.

Sherehe hiyo, iliyofanyika kwa munasaba wa Maulidi ya Mtume Muhammad al Mustafa SAW, ilihudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu wa Iran, wawakilishi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) pamoja na wasomi na wanasayansi mashuhuri wapatao sitini kutoka nchi mbali mbali za Kiislamu.

Washindi wa Awamu ya Pili ya Tuzo ya Sayansi ya Mustafa SAW walikuwa ni Profesa Sami Erol Gelenbe, mwanasayansi wa kompyuta kutoka Uturuki na Profesa Amin Shukrullahi, ambaye ni mtaalamu wa hisabati na sayansi ya kompyuta kutoka Iran.

Profesa Gelenbe akipokea Tuzo ya Mustafa SAW ya mwaka 2017 kutokana na utafiti wake wenye ubunifu wa kipekee katika uga wa sayansi na teknolojia hasa katika uga wa “Communications: Raptor Codes.”

Akizungumza katika halfa hiyo, Mahdi Safarinia, Katibu wa Baraza la Sera katika Tuzo ya Sayansi ya Mustafa SAW amesema tuzo hiyo inalenga kuunga mkono na kustawisha sayansi na teknolojia kote duniani hasa katika nchi za Kiislamu ili ziweze kufikia viwango vya kimataifa.Washindi wa Tuzo ya Sayansi ya Mustafa SAW Waenziwa Tehran

"Tuzo ya Sayansi ya Mustafa SAW inaweka msingi wa kurejesha Zama za Dhahabu katika Ulimwengu wa Kiislamu". Hizi ni zamba ambazo Waislamu waliweza kuweka misingi ya taaluma mbali mbali za kisayansi duniani katika kipindi ambacho bara ulaya lilikuwa katika kiza kielimu.

Tuzo ya Sayansi ya Mustafa SAW (The Mustafa (PBUH) Prize) ilitolewa mara ya kwanza mwaka 2015 mjini Tehran ambapo wakati huo washindi walikuwa ni Preofesa Omar Yaghi wa Jordan, mtaalamu wa nanoteknolojia na Profesa Jackie Ying wa Singapore katika uga wa bio-nanoteknolojia.

 

3464601

captcha