IQNA

Magaidi 19,000 wa ISIS wameuawa Iraq katika kipindi cha miaka 3

11:55 - March 15, 2018
Habari ID: 3471429
TEHRAN (IQNA)- Zaidi ya magaidi 19,000 wa ISIS (Daesh) wameuawa Iraq katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, amesema mkuu wa polisi nchini humo.

"Hadi sasa magaidi wapatao 19,484 wameuawa katika maeneo ya Nineveh, Kirkuk, Salahudin, Kaskazini mwa Baghdad na Anbar," amesema Luteni Jenerali Shaker Jawdat, Kamanda wa Polisi ya Iraq.

Maelefu ya magaidi hao wa ISIS waliuawa wakati serikali ya Iraq, ikishirikiana na jeshi la kujitilea la wananchi, Hashdu Shabi, lilipoanzisha oparesheni dhidi ya ugaidi Oktoba mwaka 2016.

Mwezi Disemba mwaka jana, Waziri Mkuu wa Iraq Haider al Abadi alitangaza rasmi kuangamizwa kundi la kigaidi la ISIS nchini humo baad aya maeneo yote yaliyokuwa yametekwa na kundi hilo kukombolewa.

Mapema wiki hii pia Waziri Mkuu wa Iraq alisema kwa mtazamo wa kijeshi, ugaidi umeshindwa na kumalizika nchini Iraq na sasa hatua inayofuata ni kukabiliana na fikra za kigaidi.

Aliongeza kuwa: "Leo silaha ambazo Iraq inamiliki si za kutekeleza hujuma za kijeshi bali ni kwa ajili ya kufikia amani na ujenzi mpya wa nchi ".

Al Abadi aidha amesema, dikri aliyosaini ya kuingiza vikosi vya kujitolea vya wananchi, Al-Hashd Al-Shaabi, katika vikosi vya usalama vya Iraq ni kwa lengo la kuwaunga mkono wananchi wa Iraq.

Siku ya Alhamisi, Al Abadi alitia saini dikrii rasmi ya kujumuishwa Al-Hashd Al-Shaabi katika vikosi vya usalama vya Iraq.

3465382/

captcha