IQNA

Katika kipindi cha mwaka moja

Saudia yasambaza nakala milioni 18 za Qur'ani kwa lugha mbali mbali

12:34 - September 13, 2018
Habari ID: 3471669
TEHRAN (IQNA)- Kituo cha Uchapishaji Qur'ani cha 'Malik Fahad' nchini Saudi Arabia kimetangza kuwa kimesambaza nakala milioni 18 za Qur'ani Tukufu mwaka uliopita wa Hijria Qamaria.

Katika taarifa, kituo hicho kilichoko mjini Madina kimesema katika mwaka uliopita wa 1439 Hijria Qamaria, kilifanikiwa kusambaza nakala hizo milioni 17 ambazo zimetarjumiwa kwa lugha mbali mbali.

Taarifa hiyo imesema tokea Kituo cha Uchapishaji Qur'ani cha  'Malik Fahad' kifunguliwe mwaka 1405 Hijria Qamaria hadi kufikia Dhul Hijja mwaka jana, kimeweza kuchapisha nakala milioni 310 za Qur'ani Tukufu.

3746474

captcha