IQNA

Kongamano kuhusu changamoto za tarjuma ya Qur'ani lafanyika Morocco

11:19 - December 02, 2018
Habari ID: 3471758
TEHRAN (IQNA)-Kongamano la kimataifa kuhusu changamoto katika kazi ya tarjuma ya Qur'ani limefanyika Casablanca, Morocco hivi karibuni.

Wanazuoni na watafiti kutoka Morocco, Mauritania, Misri, Tunisia, Ubelgiji na Algeria walihudhuria kongamano hilo ambalo lilifanyika Jumatano na Alhamisi.

Moja kati ya masuala yaliyojadiliwa kwa kina katika kongamano hilo ni utumizi wa maneno kama vile Jihad, Ummah na Qital katika lugha ya Kiarabu na lugha nyinginezo.

Washiriki pia walitoa wito kwa nchi za Waislamu duniani kuanzisha mpango mkubwa wa kutarjumu na kufasiri Qur'ani katika lugha mbali mbali.

Halikadhalika washiriku walitaka kuwepo jitihada maalumu za kukabiliana na njama za mustashriqin– (au orientalists kwa Kiingereza) ambao wamekuwa wakipotosha taswira ya Uislamu na Qur'ani.

3768177

captcha