IQNA

Mauaji Ndani ya Msikiti Afrika Kusini

14:03 - December 08, 2018
Habari ID: 3471764
TEHRAN (IQNA)- Mtu mmoja amepigwa risasi na kuuawa nje ya msikiti katika mtaa wa Springs, mji wa Ekurhuleni eneo la East Rand mkoani Gauteng Afrika Kusini.

Polisi katika mkoa wa Guateng wanasema mtu huyo alikuwa amemaliza kuswali Sala ya Ijumaa na alikuwa anaelekeoa aliokoegesa ghari lake wakati alipokumbana na watu wawili wasiojulikana waliomfyatulia risasi mara kadhaa. Washukiwa hao walitumia gari aina ya VW Polo kutoroka.

Mwislamu huyo aliyekuwa na umri wa miaka 30 alikimbizwa hospitalini na kufariki baadaye kutokana na majeraha aliyoyapata.

"Bado haijaweza kubainika lengo la mauaji na polisi wanawasaka washukuwa," amesema afisa mwandamizi wa polisi Kepteni Mavela Masondo katika taarifa siku ya Ijumaa.

Ikumbukwe kuwa mwezi Novemba, Mwislamu aliyekuwa na umri wa miaka 30 alipigwa risasi na kuuawa na imamu kujeruhiwa katika hujuma ndani ya msiki mjini Cape Town. Mwezi Juni pia Waislamu wawili waliuawa katika hujuma ndani ya msikiti wa Malmesbury mjini Cape Town.

Kwingineko polisi wamewaondoa tuhumani watu saba kati ya 19 waliokamatwa kufuatia hujuma dhidi ya msikiti wa Verulam nje ya Durban mapema mwaka huu. Watu hao walikamatwa baada ya shambulizi la mwezi Mei wakati watu wasiojulikana waliuhujumu Msikiti wa Imam Hussein AS katika eneo la Ottawa, Verulam, kaskazini mwa Durban na kumuua Abbas Essop.

Katika hujuma hiyo eneo moja la msikiti huo lilitekektezwa moto na bomu ambayo ilikuwa haijalipuka ilipatikana katika jingo hilo la msikiti siku chache baadaye.

3467401

captcha