Abdul Qader Gilani anasema amefanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu katika kipindi cha miezi 15. Hivi sasa anawasaidia wafungwa wenzake katika Gereza ya Konya kuhifadhi Qur'ani Tukufu.
"Wakati nilipohukumiwa kifungo cha miezi 18 gerezani, nilifahamu kuwa kuna nukta chanya katika hujumu hiyo," amesema.
"Kwa sasa, nimeamua kuwa Hafidh wa Qur'ani Tukufu. Kabla ya kuwa Hafidh sikuwa nadhani kuwa naweza kupata mafanikio hayo."
Aidha amewapongeza wakuu wa gereza kwa musaidia katika njia yake ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.
3469590