IQNA

Wanaotekeleza ibada ya Hija wawasili Makka + Video

23:17 - July 27, 2020
Habari ID: 3473007
TEHRAN (IQNA) – Waislamu wanaotekeleza ibada ya Hija wamewasilia katika mji mtakatifu wa Makka kutoka maeneo mbali mbali ya Saudi Arabia huku kukiwa na hatua kali za kuzuia kuenea ugonjwa wa corona.

Hija ya mwaka huu ni ya aina yake kwani ni Waislamu takribani 1,000 tu watakaotekelza Ibada ya Hija kufuatia uamuzi wa utawala wa Saudia kupunguza idadi ya mahujaji ili kuzuia kuenea ugonjwa wa corona. Kwa kawaida kila mwaka Waislamu takribani milioni mbili na nusu kutoka kila kona ya dunia hutekeleza ibada ya Hija lakini mwaka hii ni watu 1000 tu ambao ni raia 300 wa Saudia na raia 700 wa kigeni wanaoishi Saudia.

3912872

Kishikizo: hija waislamu saudia Corona
captcha