IQNA

Watalii wa kigeni wamiminika katika Msikiti wa Hagia Sophia

15:05 - July 30, 2020
Habari ID: 3473015
TEHRAN (IQNA) – Baada ya msikiti wa Hagia Sophia kufunguliwa mjini Istanbul, Uturuki, idadi kubwa ya watalii wa kigeni na wa ndani ya nchi wamefika katika msikiti huo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Antolia, maelfu ya watalii wa kigeni na wa ndani ya nchi wamefika katika Msikiti wa Hagia Sophia ambao jengo lake lilibadilishwa hivi karibuni kutoka matumizi kama Jumba la Makumbusho hadi Msikiti.

Watalii wa kigeni wasiokuwa Waislamu wanautembelea msikiti huo baada ya swala za kila siku.,

Swala ya kwanza ya Ijumaa iliswaliwa katika Msikiti wa Hagia Sophia, Istanbul Uturuki baada ya zaidi ya miaka 86 ambapo maelfu ya waumini wameshiriki katika swala hiyo mnamo Julai 24, 2020.

Mapema mwezi huu,  Mahakama ya juu zaidi nchini Uturuki iliidhinisha jumba la makumbusho la Hagia Sophia kugeuzwa kuwa msikiti na kubadilisha hadhi yake ya sasa kama jumba la makumbusho.

Baraza la kitaifa la Uturuki lilikubali ombi la mashirika kadhaa yakiliomba kufuta uamuzi wa serikali wa tangu mwaka 1934 unaolipa jumba la Hagia Sophia huko Istanbul hadhi ya jumba la makumbusho.

Jumba la Hagia Sophia ni miongoni mwa maeneo yaliyowekwa kwenye orodha ya turathi za duni na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO, na ni mojawapo ya vivutio vikuu vya watalii huko Istanbul.

Wananchi wa Uturuki na asasi za Kiislamu nchini humo zimeonyeshwa kufurahishwa na uamuzi huo wa mahakama.

3913566

captcha