IQNA

UAE yaruhusu asilimia 50 kuswali misikitini

19:16 - August 02, 2020
Habari ID: 3473025
TEHRAN (IQNA)- Misikiti katika Umoja wa Falme za Kiarbau (UAE) itaruhusiwa kuwa na asilimia 50 ya idadi ya wanaoweza kuswali ndani yake kuanzia Agosti 3.

Uamuzi huu unaufatia ule wa Julai 1 wa kuruhusu kila msikiti kuruhusiwa kuwa na asilimia 30 ya waumini wanaoweza kuswali humo wakati wa swala. Misikiti ya UAE ilifunguliwa Julai 1 baada ya kufungwa kwa miezi kadhaa kutokana na kuenea ugonjwa ambukizi wa corona.

Kwa mujibu wa kanuni mpya wanaswali msikitini wanapaswa kudumisha umbali wa mita mbili baina yao na muda baina ya adhana na iqama usizidi dakika 10 isipokuwa wakati wa swala ya Magharibi ambapo muda huo utakuwa ni dakika tano.

Waumini katika maeneo ya ibada yaliyofunguliwa wametakiwa kuzingatia kanunu zilizowekwa za kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19. Aidha wazee, watoto wenye umri wa miaka 12 na wale wenye magonjwa sugu wametakiwa wasifike misikitini. Halikadhlika baadhi ya misikiti itaendelea kufunguwa. Misikiti hiyo ni ile iliyo kando ya barabara, misikiti iliyo katika maeneo ya viwanda na kumbi za swala katika maduka makubwa (mall).

3472164

captcha