IQNA

Rais Raisi wa Iran katika hotuba kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

Sera za ubeberu za Marekani na waitifake wake zimefali, hazina itibari kimataifa

12:24 - September 22, 2021
Habari ID: 3474324
TEHRAN (IQNA)- Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema juhudi za Marekani na washirika wake za kuitwisha dunia ubeberu wao zimefeli vibaya na kwamba siasa hizo za ubeberu hazina itibari tena kimataifa.

Akihutubia kikao cha 76 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza tangu aingie madarakani mwezi uliopia, Jumanne usiku kupitia mawasiliano ya video, Rais Raisi amesema matukio mawili makuu yameweka historia mpya mwaka huu, moja likiwa ni lile lililotokea tarehe 6 Januari huko Marekani ambapo magenge ya wahuni yalivamia Congress ya Marekani na jingine ni kudondonshwa mwezi Agosti kutoka angani kwenye ndege za Marekani, raia wa Afghanistan. Raisi amesema katika hutoba yake hiyo kwa Baraza Kuu la Umoja wa Matifa kwamba jambo lililothibiti katika matukio mawili hayo ni kuwa ubeberu wa Marekani, uwe ndani au nje ya nchi, hauna tena itibari. Ameendelea kusema: 'Matokeo ya kuenezwa ubeberu duniani ni umwagaji damu na kuvurugwa amani na usalama na hatimaye kushindwa na kukimbia. Leo, Marekani haitafuti tena kutoka bali inafukuzwa Iraq na Afghanistan.'

Raisi amesema Marekani inatumia vikwazo kama 'mbinu mpya ya vita' dhidi ya mataifa mengine na kusisitiza kwamba vikwazo vya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kipindi hiki cha kuenea duniani virusi hatari vya corona ni 'jinai dhidi ya binadamu'.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Rais Raisi amesema kwamba Iran imekuwa na ingali inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa mapatano ya nyuklia ya mwaka 2015 mashuhuri kama JCPOA, katika hali ambayo Marekani ilivunja ahadi zake katika mapatano hayo na kisha kuanza kutekeleza mashinikizo ya juu dhidi ya Iran, mashinikizo ambayo hata hivyo amesema yameshindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa. Raisi amesema Iran haitaki chochote cha ziada ghairi ya kupatiwa haki zake na kuheshimiwa sheria za kimataifa na hasa zinazohusiana na mapatano ya nyuklia na maazimio ya Umoja wa Mataifa.

Rais wa Iran amesema ripoti 15 zilizotolewa na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA zinathibitisha wazi kwamba Iran imetekeleza ahadi zake zote kwa mujibu wa mapatano ya JCPOA bali ni Marekani ndio imekiuka ahadi na majukumu yake katika uwanja huo.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kwamba Iran haina imani na ahadi zinazotolewa na Marekani na kwamba la muhimu ni kufutiliwa mbali mara moja vikwazo vya kidhalimu vilivyowekwa na nchi hiyo dhidi ya watu wa Iran. Amesema Iran itayapa umuhimu mazungumzo ya nyuklia iwapo tu yatapelekea kuondolewa vikwazo hivyo vya upande mmoja.

Rais Donald Trump wa Marekani aliitoa nchi hiyo katika mapatano ya JCPOA mwaka 2018 na kurejesha vikwazo ambavyo vilikuwa vimeondolewa dhidi ya Iran kwa mujibu wa mapatano hayo.

3999221

captcha