IQNA

Wayemen washiriki maandamano makubwa ya kuadhimisha mapinduzi yao

12:56 - September 22, 2021
Habari ID: 3474326
TEHRAN (IQNA)- Idadi kubwa ya wananchi wa Yemen Jumanne wamefanya maandamano makubwa katika mkoa wa Saada wa kaskazini wa nchi hiyo kwa mnasaba wa maadhimisho ya tarehe 21 Septemba, siku ya mapinduzi ya nchi hiyo.

Televisheni ya al Masirah imetangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, waandamanaji wamebeba picha za Sayyid Abdul Malik Badruddin al Houthi, Kiongozi Mkuu wa harakati ya Ansarullah ya Yemen ili kuadhimisha mapinduzi ya wananchi wa nchi hiyo ya Kiarabu.

Mwaka 2014 katika siku kama ya leo, wananchi wa Yemen walifanya mapinduzi yaliyoing'oa madarakani serikali ya vibaraka wa Saudi Arabia.

Tangu mwaka huo hadi hivi sasa wananchi wa Yemen wanaadhimisha siku hiyo kila mwaka kwa jina la siku ya ukombozi.

Mwezi Machi 2015, Saudi Arabia ilianzisha mashambulizi makubwa ya kivamizi dhidi ya wananchi wa Yemen kwa uungaji mkono kamili wa Marekani, utawala wa Kizayuni wa Israel, madola mengine ya kibeberu ya Marekani na kwa ushirikiano mkubwa na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) na baadhi ya nchi za Kiarabu kama Sudan.

Tangu wakati huo hadi hivi sasa madola hayo vamizi yameizingira kila upande Yemen kutokea angani, baharini na ardhini na hawaruhusu chochote kuingia wala kutoka nchini humo. Hiyo ni jinai nyingine kubwa inayofanywa na wavamizi wa nchi ya Kiislamu ya Yemen.

Hadi hivi sasa uvamizi huo wa Saudia na kundi lake umeshasababisha makumi ya maelfu ya Wayemen kuuawa, wengine wengi kujeruhiwa huku mamilioni ya wengine wakiwa wakimbizi ndani na nje ya nchi.

برگزرای راهپیمایی بزرگداشت انقلاب ۲۱ سپتامبر در یمن

برگزرای راهپیمایی بزرگداشت انقلاب ۲۱ سپتامبر در یمن

برگزرای راهپیمایی بزرگداشت انقلاب ۲۱ سپتامبر در یمن

برگزرای راهپیمایی بزرگداشت انقلاب ۲۱ سپتامبر در یمن

برگزرای راهپیمایی بزرگداشت انقلاب ۲۱ سپتامبر در یمن

 

3999218

captcha