IQNA

Misikiti ya Oman yaanza tena Sala ya Ijumaa

20:45 - September 23, 2021
Habari ID: 3474328
TEHRAN (IQNA)- Misikiti ya Oman imeidhinishwa kuanza tena Sala za Ijumaa baada ya kufungwa kwa muda wa mwaka moja na nusu kutokana na janga la maambukizi ya COVID-19.

Hivi sasa kufuatia  kupungua maambukizi ya COVID-19 na pia kupungua  kwa kiwango kikubwa idadi ya wanaopoteza maisha kutokana na ugonjwa, huo, Kamati Kuu ya Kukabiliana na COVID-19 imetangaza kuwa misikiti itaruhusiwa kuwa na Sala ya Ijumaa kuanzia Septemba 24.

Idhini hiyo hiyo imetolewa kwa masharti ambapo wale tu waliopata chanjo ya COVID-19 ndio watakaoruhusiwa kushiriki katika Sala ya Ijumaa.  Aidha wanaosiriki katika Sala ya Ijumaa wanatakiwa kuzingatia kanuni za kukabiliana na COVID-19 kama vile kutokaribiana, kila moja kubeba mkeka binafsi wa kusali, kuvaa barakoa na wanaosalia msikiti wasizidi asilimia 50 ya idadi inayoruhusiwa.

3475768

Kishikizo: oman covid 19 ijumaa sala
captcha