IQNA

Sheikh Sabri atahadharisha kuhusu njama mpya za Wazayuni dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa

22:33 - September 24, 2021
Habari ID: 3474335
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Msikiti wa al-Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) amesisitiza kuwa, hatua ya Wazayuni ya kung'ang'a kuingia kinyume cha sheria katika Msikiti wa al-Aqsa inaweka wazi njama zao za kutaka kutwisha uhakika mpya kuhusiana na kibla hicho cha kwanza cha Waislamu.

Sheikh Ekrima Sa'id Sabri amesema kuwa, bila ya himaya na uungaji mkono wa wanajeshi vamizi wa Israel, walowezi wa Kizayuni hawawezi kuthubutu kuingia katika Msikiti wa al-Aqsa, na hilo linaonyesha kuwa, wanaogopa hasira za wakazi wa Quds ambao ndio wamiliki asili wa maeneo matakatifu katika mji huo.

Khatibu wa Msikiti wa al Aqsa amesisitiza kuwa, viongozi wa utawala haramu wa Israel wamekuwa wakitoa himaya na uungaji mkono kamili kwa walowezi wa Kizayuni ambao wamekuwa wakifanya hujuma mara kkwa mara na kuingia  katika Msikiti wa al-Aqsa na kulivunjia heshima eneo hhilo takatifu.

Vitendo vya chuki na uadui vya walowezi wa Kizayuni vimeendelea baada ya jana mamia ya walowezi hao wenye chuki na Uislamu kuuvamia Msikiti wa al-Aqsa ambao ndicho Kibla cha Kwanza cha Waislamu.

Sheikh Ekrima Sabri alinukuliwa pia majuzi akisema kuwa, kuwa, Israel imetumia vibaya matukio mbalimbali kwa ajili ya kuudhibiti Msikiti wa al Aqsa lakini njama hizo zimefeli kutokana na kusimama kidete na mapambano ya taifa la Palestina linalosisitiza kuwa msikiti huo ni milki ya Waislamu.

Katika wiki za karibuni walowezi wa Kizayuni wakisaidiwa na askari wa utawala haramu wa Israel wamezidisha hujuma na mashambulizi dhidi ya Msikiti wa al Aqsa na maeneo ya kandokando yake wakiwa na lengo la kuwalazimisha Waislamu kuyahama maeneo hayo.   

3478114

captcha