IQNA

Msomi wa Lebanon

Kuna haja ya kuwa na sheria ya kimataifa kuuhami Umoja wa Kiislamu

11:43 - November 30, 2021
Habari ID: 3474620
TEHRAN (IQNA)- Mwanazuoni maarufu wa Kiislamu nchini Lebanon amesema kuna haja ya kupitishwa sheria za kimataifa ambazo zinapiga marufuku uibuaji mifarakano na migongano baina ya wafuasi wa madhehebu mbali mbali za Kiislamu.

Katika mahojiano na IQNA, Sheikh Ghazi Hanina, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maulamaa Waislamu Lebanon amesema katika nchi za Magharibi wale ambao kwa mfano kuna sheria za kupiga marufuku dhidi ya Mayahudi na wale wanaokiuka sheria hizo wanaadhibiwa. Ameongeza kuwa, "Hadi sasa hatujaona hatua zozote za kivitendo zikichukuliwa na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) au Jumuiya ya Nchi za Kiarabu au mabaraza yoyote mengine katika nchi za Kiislamu kuzuia mauaji ya Waislamu."

Aidha amebainisha masikitiko yake kuwa baadhi ya mitandao ya kijamii imegeuka na kuwa vituo vya kueneza mifarakano na hitilafu baina ya Waislamu badala ya kueneza elimu na muongozo.

Halikadhalika amesema baadhi ya vituo vya televisheni vinatumika kuhimiza itikadi za ukufurushiaji na mifarakano baina ya Waislamu na kupelekea kuuawa Waislamu wasio na hatia katika nchi kama vile Afghanistan, Syria na Yemen.

Sheikh Hanina amesema moja ya nukta ambazo zinaweza kuleta nguvu katika Umma wa Kiislamu  na kuongeza kuwa, chanjo cha umoja ni imani kwa Allah SWT, Mtume Muhammad SAW na Qurani Tukufu.

Mwanazuoni huyo wa Kiislamu Lebanon amesema kati ya changamoto za kufikia umoja wa Waislamu ni hitilafu za kifiqhi. Amesema Katika zama za awali za Uislamu, hitilafu hizo za kina zilikuwa zikijadiliwa na wasomi katika vituo vya utafiti wa Kiislamu na hazikuwa mada za kujadiliwa kila mahala.

captcha