IQNA

Njama dhidi ya Iran

Uingereza na Marekani zimehusika moja kwa moja kuchochea machafuko nchini Iran

19:58 - October 01, 2022
Habari ID: 3475864
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Usalama ya Iran imesema Marekani na Uingereza zilichochea ghasia zilizoshuhudiwa hivi karibuni kote Iran.

Katika taarifa ya Ijumaa, Wizara hiyo imeongeza kuwa makumi ya magaidi wanaofungamana na utawala wa Kizayuni wa Israel na makundi ya wanaopinga mapinduzi ya Kiislamu wamekamatwa katika oparesheni za kiusalama hivi karibuni.

Wizara hiyo imesisitiza kuwa kumekuwepo na uchochezi wa nyuma ya pazia wa ghasia zilizojitokeza kufuatia kifo cha mwamamke mwenye umri wa miaka 22 kutoka eneo la Kurdistan kwa jina la Mahsa Amini ambaye alizimia ndani ya kituo cha polisi na kupoteza maisha hospitalini wakati akipata matibabu.

Kufuatia kifo hicho kuliibuka maandamano kote Iran ambapo waibua ghasia waliharibu mali za umma na kuteketeza moto magari ya polisi na ambulensi.

Wizara ya Usalama ya Iran imesema kulikua na makundi matatu yaliyoshiriki katika ghasia za hivi karibuni. Kwanza ni wachochezi wa kigeni, wafuasi wa kundi la kigaidi linalopinga Iran la MKO lenye makao yake Albania, na watu waliokuwa wakishirikiana na makundi ya kigaidi yanayopinga mapinduzi ya Kiislamu. Taarifa hiyo imebaini kuwa: "Katika siku za hivi karibuni, vikosi vya kulinda usalama nchini Iran vimekuwa vikikabiliana na makundi kadhaa sugu na vibaraka wa mashirika ya kijasusi ya kigeni. Aidha kumekuwepo na uingiliaji wa moja kwa moja wa serikali za Marekani na Uingereza na kwa himaya ya Saudia Arabia katika kuwahadaa walioibua ghasia mitaani."

Taarifa ya Wizara ya Usalama imesema magaidi 49 wa MKO wamekamatwa wakieneza habari feki na kuwachochea waibua ghasia washiriki katika vitendo vya kigaidi na uharibifu wa mali za umma. Aidha wafuasi 77 wa makundi ya kigaidi yanayopinga Mapinduzi ya Kiislamu wamekamatwa katika eneo la Kurdistan nchini Iraq. Taarifa hiyo imesema wafuasi watano wa makundi ya magaidi wakufurishaji wamekamatwa wakiwa na kilo 36 za mabomu ambayo yalikuwa yatumike katika mijimuiko.

Hali kadhalika maafisa wa usalama wa Iran wamewakamata watu 96 wanaofungamana na utawala wa kifalme ulioangushwa Iran wa Kipahlavi uliokuwa ukipata himaya ya Marekani. Waliokamatwa walikuwa wakichochea ghasia. Raia wa kigeni walionaswa wakichochea ghasia Iran wana uraia wa nchi tisa zikiwemo Ujerumani, Poland, Italia, Ufaransa, Uholanzi na Sweden.

Wizara ya Usalama ya Iran pia katika oparesheni zake imenasa idadi kubwa ya bunduki na risasi.

4088821

captcha