IQNA

Waliosilimu Qatar washiriki katika mashindano ya Qur’ani

18:20 - June 13, 2015
Habari ID: 3313858
Watu 183 waliosilimu na wanaoishi Qatar wamejisajilisha kushiriki katika mashindano ya kitaifa ya Qur’ani katika nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi.

Kwa mujibu wa gazeti la Al-Raya, Waislamu hao wanajumuisha wanaume 141 na wanawake 42 kutoka nchi mbali mbali duniani na watashindano katika kuhifadhi na kusoma (tarteel) sura fupi fupi za Qur’ani Tukufu.
Kamati andalizi ya mashindano ya kitaifa ya Qur’ani imetangaza kuwa, ililinganishwa na mashindano ya miaka miwili iliyopita, mwaka huu kuna washiriki 77 zaidi.
Lengo la mashindano hayo limetajwa kuwa ni kuwahimiza na kuwawezesha waliosilimu kujifunza misingi ya Qur’ani Tukufu.
Aidha mashindano hayo ya Qur’ani yanalenga kueneza thamani za Qur’ani na Kiislamu miongoni mwa  waliosilimu ili waweze kutekeleza Uislamu katika maisha yao.../mh

3312353

captcha