IQNA

Waislamu Waungane Kuvunja njama za Israel dhidi ya Al Aqsa

18:49 - August 21, 2015
Habari ID: 3349556
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesisitiza kuhusu udharura wa umoja baina ya Waislamu ili kukabiliana na njama hatari za utawala haramu wa Israel za kuubomoa Msikiti wa Al Aqsa katika Mji wa Quds (Jerusalem).

Katika taarifa iliyotoelwa siku ya Ijumaa, Wizara ya Mambo ya Nje ya Irna imekariri tena kuhusu uungaji mkono usioterereka wa Jamhuri ya Kiislamu kwa mapambano ya Wapalestina na kuongeza kuwa, umoja wa Waislamu na watu wote wapenda uhuru duniani ni jambo litakalovunja njama za Israel za kuuharibu msikiti wa al-Aqsa. Taarifa hiyo imetolewa kwa mnasaba wa  kumbukumbu ya mwaka wa 46 tokea kuteketezwa moto sehemu ya Msikiti wa al-Aqsa. Ikumbukwe kuwa manamo Agosti 21 mwaka 1969, setla Myahudi mwenye misimamo mikali akishirikiana na wanajeshi wa utawala haramu wa Israel waliteketeza moto eneo la kusini mashariki la msikiti huo ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu. Baada tukio hilo, nchi za Kiislamu zilikutana na kuamua kuunda Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) ili kukabiliana na hatari zinazoukabili ulimwengu wa Kiislamu na matukufu yake.
Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imezitaka nchi za Kiislamu kutoa msaada ya kvitendo kwa Msikiti wa Al Aqsa ambao ni chanzo cha umoja wa dini zote za mbinguni.
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran imetoa taarifa hiyo kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka wa 47 wa kuchomwa moto Masjidul Aqswa na Wazayuni. “Tarehe 21 inakumbusha tukio ambalo haliwezi kusahauliwa na ambalo licha ya kupita miaka 47 sio Waislamu tu ambao hawajalisahau bali wafuasi wengine wa dini za mbinguni nao wangali wanalikumbuka tukio hili chungu ambalo linazidi kuweka wazi jinsi wazayuni walivyobobea katika kutenda jinai na moyo wa kupenda kufanya uvamizi na hujuma."
Taarifa hiyo ya Iran pia imekosoa njama za Israel za kuvuruga mwamko na intifadha ya Wapalestina na kusema utawala wa Tel Aviv hauwezi kuzima azma ya Waislamu katika kuikomboa Quds Tukufu. Iran pia imeonya kuhusu njama  zaIsrael kuhusu za kuuyahudisha mji wa Quds na masetla wa Kizayuni wanaouhujumu Msikiti wa Al Aqsa.../mh

3347173

captcha