IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu baada ya Mauaji ya kutisha Orlando, Marekani

14:03 - June 13, 2016
Habari ID: 3470382
Watu wasiopungua 50 wameuawa na wengine 53 kujeruhiwa katika ufyatuaji wa risasi uliotokea katika jimbo la Florida nchini Marekani.

Ripoti zinasema kuwa, mashambulizi ya jana huko Orlando ni moja kati ya matukio yaliyosababisha mauaji makubwa ya ufyatuaji wa risasi katika jamii ya Marekani. Vyombo vya habari vinasema kuwa, mtu aliyefanya shambulizi hilo ni Mmarekani mwenye asili ya Afghanistan aliyejulikana kwa jina la Omar Mateen. Kutokana na wasifu uliotolewa na vyombo vya habari vya Marekani kuhusu utambulisho wa mtu huyo, kumeanzishwa wimbi kubwa la hujuma na mashambulizi dhidi ya Uislamu na Waislamu katika jamii ya nchi hiyo. Hii ni licha ya kwamba, mafundisho ya dini tukufu ya Uislamu yanakataza mauaji ya wanadamu wasio na hatia yoyote. Hata hivyo inasikitisha kuona kuwa, serikali na vyombo vya habari vya nchi za Magharibi hususan Marekani havitofautishi baina ya watu wanaofanya ugaidi kwa kutumia jina la Uislamu na mafundisho sahihi ya Qur'ani na Mtume Muhammad (saw) wakati vinapolaani na kuzungumzia ugaidi. Njama hii ya kuyahusisha na Uislamu mashambulizi yote ya kigaidi inafanyika kwa makusudi kwa shabaha ya kuharibu na kuipaka matope sura safi ya dini huyo ya Mwenyezi Mungu na wafuasi wake. Vilevile tinasisitiza kwamba, makundi ya kigaidi ambayo hii leo yanaua watu katika nchi mbalimbali ikiwemo Marekani ni matunda ya siasa za Marekani yenyewe za kuyaunga mkono na kuyasaidia makundi ya kitakfiri na kigaidi. Kwani kama si siasa za uingiliaji kati wa Marekani na kutaka kujitanua katika nchi za Kiislamu za Asia na kaskazini mwa Afrika na vilevile himaya na misaada ya Washington kwa makundi ya kitakfiri na kigaidi basi kusingekuwapo harakati na makundi hayo ya kigaidi. Utawala wa Aal Saud huko Saudi Arabia ambao ndio mfadhili mkuu wa makundi ya kitakfiri na kigaidi katika eneo la Mashariki ya Kati ni muitifaki na mshirika mkubwa zaidi wa Marekani katika eneo hilo.

Wakati huo huo mtu anayefaidika zaidi na tukio la jana huko Orlando ni Donald Tramp, mgombea mtarajiwa wa kiti cha rais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican katika uchaguzi ujao. Awali Tramp alitoa wito wa kupigwa marufuku Waislamu kuingia Marekani. Kwa msingi huo Tramp atafanya jitihada kubwa kuhakikisha kunaenea zaidi anga ya woga na hofu nchini Marekani baada ya tukio la jana huko Orlando kwa ajili ya kujipatia kura zaidi za Wamarekani.

Wakati huo huo Tramp na wenzake watachochea zaidi wimbi la hujuma na chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu katika vyombo vya habari.

Kufuatia hali hiyo, Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR) limelaani hujuma katika mji wa Orlando nchini Marekani ambapo watu wasiopungua 50 waliuawa jana katika klabu moja huku wengine 53 wakijeruhiwa.

Aliyetekeleza mauaji hayo anadaiwa kuwa muungaji mkono wa kundi la kigaidi la ISIS au Daesh.

Kundi la kigaidi la ISIS limetangaza kuhusika na hujuma hiyo. Katika taarifa, CAIR imetaja mauaji hayo kuwa ni jinai ya chuki ambayo inalaaniwa vikali. Mwenyekiti wa Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani Nihad Awad amesema mauaji hayo yanakiuka misingi ya Marekani na Waislamu. Aidha amesisitiza kuwa ISIS ni kundi haramu lisilowakilisha Waislamu.

3506521

captcha