IQNA

Zaidi ya 44 wauawa katika mapigano Kashmir inayodhibitiwa na India

19:45 - July 19, 2016
Habari ID: 3470465
Zaidi ya watu 44 wameuawa kufikia Jumanne katika mapigano yalianza Julai 9 katika eneo la Kashmir linalidhibitiwa na India.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, watu wengine 3,500 wamejeruhiwa, wengi wakiwa na majeraha ya macho, kutokana na risasi hatari lakini zisizozua zinazutumiwa na jeshi la India kuwakandamiza waandamanaji.
Mapigano ya sasa yalianza wakati, Burhan Wani , kiongozi muandamizi wa chama cha kupigania uhuru wa Kashmir, Hizb ul Mujahideen, kuuawa akiwa nwa watu wengine wawili baad aya kufyatulaina risasi na wanajeshi wa India katika eneo la Kokernag mnamo Julai 9.
Mauaji yake yaliibua ghasia kaitka mji wa Anantanag, ambapo maelfu ya waandamanaji wamekuwa wakitoa nara za kutaka uhuru. Wanajeshi wa India wametumia risasi hao, gesi ya kutoa machozi na risasi za plasitiki zisizoua kuwatawanya waandamanaji.
Mkuu wa Polisi ya India huko Kashmir, K. Rajendra Kumar amesema kuuawa, Wani ni mafanikio makubwa katika vita dhidi ya wanamgambo Kashmir. Aidha amejigamaba kuwa polisi wameua wanamgambo 83 huko Kashmir mwaka huu pekee.
Kashmir ni jimbo lenye Waislamu wengi India na limekuwa lilikumbwa na mzozo tokea India ipate uhuru kutoka Uingereza mwaka 1947. Eneo linguine la Kashmir liko Pakistan ambayo pia ilikuwa koloni la Uingereza.  Aghalabu ya Wakaazi wa Kashmir inayokaliwa na India wanataka kujitenga huku wengine wakitaka kujiunga na Pakistan. India na Pakistan zimewahi kupigana mara tatu kwa ajili ya Kashmir ambapo nchi mbili zilitiliana saini mapatano ya usitishwaji via mwaka 2003.
Wakati huo huo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa wito kwa utulivu baina ya pande hasimu katika Kashmir inayodhibitiwa na India. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Bahram Qassem amesema mzozo wa Kashmir unaweza kutatuliwa kwa njia za Amani na mazungumzo.
/3460445

Kishikizo: kashmir india iqna waislamu
captcha