IQNA

Vituo vya Kutafakari Qur'ani kwa wafanyaziara ya Arubaini

15:03 - November 16, 2016
Habari ID: 3470679
IQNA-Vituo maalumu vya kutafakari kuhusu Qur'ani Tukufu vimetengwa katika njia zinazotumiwa na wafanyaziara wanaoekelea Karbala kwa ajili ya Arubaini ya Imam Hussein AS.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, vituo hivyo maalumu kwa wanawake vimewekwa katika njia zote za kuelekea Karbala ambapo wafanyaziara watapata fursa ya kutulia na kutafakari kuhusu aya za Qur'ani Tukufu.

Mmoja wa wahusika wa mpango huo, Fatima Ismail amesema Ziara ya Siku ya Arubaini ni fursa kwa ajili ya kustawisah utamaduni wa kutafakri kuhusu aya za Qur'ani.

Amesema wanawake wanaosimama katika vituo hivyo kutafakari kuhusu Qur'ani baadaye watakuwa mabalozi wa kueneza utamaduni wa Qur'ani katika jamii zao.

Wanoshukia katika vituo hivyo wanasoma aya kadhaa a Qur'ani, kanunu za tajwidi na kusha kujadili masuala ya kifiqhi n.k

Inafaa kukumbusha hapa kuwa, majlisi na ziara ya siku ya Arubaini hufanyika kila mwaka tarehe 20 Safar, kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Qamaria,  baada ya kupita siku Arubaini tangu tarehe 10 mwezi wa Muharram kwa ajili ya kukumbuka kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume SAW, Imam Hussein AS na masahaba zake ambao walijitolea roho zao kwa ajili ya kuhuisha dini ya Mwenyezi Mungu katika jangwa la Karbala.

3546222

captcha