Taarifa zinasema watu wasiojulikana wameweka kichwa cha
nguruwe katika eneo la msikiti unaojengwa na Jumuiya ya Waislamu wa Uturuki
ijulikanayo kama Ditib. Kumekuwepo na upinzani mkali wa ujenzi wa mji huo.
Taarifa zinasema wakaazi wa mji huo wameandamana mara kadhaa kupinga ujenzi wa
msikiti huo wakitaka leseni yake ibatilishwe.
Jumuiya ya Waislamu wa Uturuki inafadhili misikiti 900 kote
Ujerumani, nchi ambayo ina Waislamu milioni tatu wenye asili ya Uturuki.
Katika miaka ya hivi karibuni kumeshuhudiwa ongezeko kubwa
la chuki dhidi ya Waislamu huku chama cha AfD kinachopinga Waislamu kikipata
asilimia 13 ya kura katika uchaguzi wa mwezi jana nchini humo.
3656999