Maandamano hayo ambayo yamefanyika katika Medani ya Tahrir mjini Baghdad ikiwa inakaribia mwaka moja tokea Marekani itekeleza hujuma ya kigaidi iliyopelekea makamanda hao kuuawa.
Katika maandamano hayo ambayo aghalabu ya washiriki wake walikuwa ni wanamapambano wa Jeshi la Kujitolea la Wananchi maarufu kama Hashd al Sha’abi waandamnaji wamelaani vikali ugaidi wa Marekani .
Luteni Jenerali Qassem Soleimani aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) alielekea Iraq kufuatia mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo aliuawa shahidi tarehe 3 Januari mwaka huu katika shambulio la anga la wanajeshi vamizi na magaidi wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad Iraq akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq (Hashdu Shaabi) na wenzao wanane. Kamanda Soleimani alikuwa safarini nchini Iraq kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo.