Katika agizo jipya, misikiti kote Misri itarejea katika hali ya kawaida ya ibada ambapo pia kutakuwa na darsa za Qur'ani, mihadhara ya kidini na ziara katika maeneo matakatifu bila vizingiti.
Msikiti Mtakatifu wa Imam Hussein AS pia utakuwa wazi kwa waumini nyakati zote za siku. Halikadhalika kumbi za sala za wanawake nazo pia sasa zitafunguliwa baada ya kufungwa kwa miaka miwili.
Uamuzi huo umechukuliwa baada ya Waziri wa Wakfu Sheikh Mokhtar Gomaa kuwasilisha mapendekezo kwa wizara ya mambo ya ndani kufuatia kupungua maambukizi ya corona nchini Misri.