IQNA

Harakati za Qur'ani

Serikali ya Jordan yatakiwa ifungue tena vituo vya Qur’ani

22:30 - July 13, 2022
Habari ID: 3475497
TEHRAN (IQNA) – Wito unaendelea kutolea nchini Jordan wa kubatilisha hatua ya serikali ya kufunga vituo 68 vya Qur’ani nchini humo.

Hivi karibuni Wizara ya Wakfu ya Jordan ilivifunga vituo hivyo kwa kutozingatia masharti mapya yaliyowekwa na wizara hiyo yanayoweka vizingiti katika shughuli za vituo vya Qur'ani na Kiislamu.

Ibrahim al-Minsi, kiongozi wa harakati moja kisiasa wa Kiislamu nchini Jordan, alielezea sababu zilizotangazwa za kufunga vituo hivyo kuwa hazikubaliki.

Alisema wizara hiyo imeanzisha vikwazo vipya na hivi karibuni ilivifunga vituo hivyo kwa kutokidhi viwango hivyo.

Hii sio hatua ya busara, al-Minis alisema katika chapisho kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii.

Amesema muda ufaao unapaswa kutolewa kwa vituo vya Qur'ani ili zijiandae kuhakikisha shughuli zao zinaendana na kanuni mpya.

Alitoa wito wa upatanishi na mazungumzo ili wizara ishawishike kufikiria upya uamuzi wake.

Wakati huo huo, Mohammad Zakhar al-Majali, mjumbe wa baraza la utawala la Jumuiya ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu ya Jordan, alisema kufungwa kwa vituo hivyo ni hatua ya muda.

Serikali imetangaza vizuizi kama vile kupunguza masaa ya kazi ya vituo na masharti ya wasimamizi na walimu.

Wale walio tayari kufundisha katika vituo hivyo sasa wanahitaji kufaulu mitihani inayotayarishwa na Wizara ya Wakfuna Masuala ya Kiislamu.

Wanaharakati wanasema kukidhi baadhi ya masharti yaliyoletwa haiwezekani kwa sababu aghalabu ya vituo hivi hutegemea walimu na wafanyakazi wa kujitolea.

4070476  

Kishikizo: qurani tukufu jordan
captcha