IQNA

Kuhifadhi Qur’ani

Msichana aliyehifadhi Qur’ani New Jersey Marekani aenziwa

21:17 - August 02, 2022
Habari ID: 3475569
TEHRAN (IQNA)- Msichana aliyehifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu huko New Jersey Marekani ameenziwa kutokana na mafanikio yake.

Safoorah Ali, mwenye umri wa miaka 11 ameenziwa Jumatatu kutokana na jitiahda zake zilizoanza miaka minne iliyopita. Wakati wa janga la corona, mama yake ambaye amehifadhi Qur’ani ndiye aliyechukua jukumu la kumsaidia kuhifadhi Qur’ani.

“Mama yangu ambaye pia naye amehifadhi Qur’ani alinipa motisho na kunisaidia sana,” amesema.

Naye mama yake, Daktari Anjum Chatha amesema: “Tunahisi tumebarikiwa sana kuwa na binti ambaye ameweza kuhifadhi Qur’ani.”

Shangazi yake, Rahat Chatha, naye anasema msichana huyo amepata mafanikio makubwa na jitihada zake ni mfano wa kuigwa na wengine.

3479944

captcha