IQNA

Waislamu India

Waislamu laki mbili wa India kuruhusiwa kushiriki Ibada Hajj ya 1444: Ripoti

21:47 - December 10, 2022
Habari ID: 3476228
TEHRAN (IQNA) - Kamati ya Hijja ya India imeripotiwa kutangaza kwamba mahujaji laki mbili wataruhusiwa kuhiji mnamo mwaka huu wa 1444 Hijria Qamarai sawa na 2023.

Matangazo rasmi katika suala hili yatatolewa hivi karibuni. Hii itakuwa ni kwa mara ya kwanza kwa Waislamu laki mbili kutoka India kutekeleza ibada ya Hija.

Mjumbe wa Kamati ya Hija ya India (HCoI) Aijaz Hussain alisema kuwa baada ya mashauriano ya kina na Wizara ya Hijja ya Serikali ya Saudi Arabia, imeamuliwa kuwa Mahujaji laki mbili kutoka India watatekeleza Ibada ya Hija mwaka huu wa Hijria Qamaria. “Idadi ya wanaotekeleza Hija imeongezwa na kwa mwaka 2023, Mahujaji laki mbili watatekeleza ibada takatifu ya Hija,” alisema. "Katika Hajj 2023, lengo maalum litakuwa kwa mahujaji wanawake."

Alisema kuwa HCoI tayari imechukua hatua kuwezesha Mahujaji kutekeleza ibada hiyo kwa njia ya kuridhisha. "

Baada ya kuanza tena Hija mwaka huu wa 2022 baada ya miaka miwili kusitishwa kwa sababu ya janga la Covid, ni Waislamu 80,000 pekee wa India waliohiji.

3481608

Kishikizo: india ibada ya hija
captcha