IQNA

Kongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kuwaunga mkono kwa kila namna Wapalestina

21:23 - February 18, 2023
Habari ID: 3476581
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezikosoa nchi za Kiislamu kwa kutochokua hatua yoyote ya maana juu ya kadhia ya Palestina.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, "Palestina ingali kadhia kuu kwa umma wa Kiislamu. Taifa hilo limewekewa mzingiro kikamilifu na watu wasio wa kawaida, bali na kundi la watu waovu na mafasiki; hata hivyo nchi za Kiislamu zimeendelea kuwa watazamaji tu."

Kiongozi Muadhamu ameyasema hayo leo Jumamosi hapa Tehran katika mkutano wake na maafisa pamoja na wajumbe wa nchi za Kiislamu wanaoshiriki kwenye Mashindano ya Kimataifa ya Qurani Tukufu. Mashindano hayo yamefanyika kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kubaathiwa na kupewa Utume, Mtume Muhammad (SAW).

Ayatullah Ali Khamenei amebainisha kuwa, kuendelea kufumbia macho na kunyamazia matatizo ya Wapalestina, na hata kushirikiana na utawala huo wa Kizayuni unaozikaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina kumezidhoofisha nchi za Kiislamu.

 

Kiongozi Muadhamu ameyakosoa baadhi ya madola ya Kiarabu kwa kushindwa kusimama kidete mkabala wa utawala haramu wa Israel na kusisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu itaendelea kuwaunga mkono kwa kila namna wananchi madhulumu wa Palestina. Aidha amesema chuki dhidi ya Iran zinatokana na hatua ya Iran kuendelea kuunga mkono Palestina.

Amefafanua kwa kusema: Kusalia kimya juu ya kadhia ya Palestina kumeudhuru ulimwengu wa Kiislamu. Kimya hicho cha serikali za Kiislamu mkabala wa uvamizi huo, ambao ni uvamizi pia dhidi yao na umma wa Kiislamu, na hata kuunga mkono (uvamizi huo), na baadhi wamefanya hivyo hivi karibuni, kumezidhoofisha nchi hizo na hata kuziweka katika madhila.

Ayatullah Khamenei amebainisha kuwa, iwapo serikali za Kiislamu zingelisimama kidete juu ya kadhia ya Palestina tokea mwanzo na wapambane, basi hali katika eneo la Asia Magharibi bila shaka ingelikuwa tofauti, na umma wa Kiislamu leo hii ungelikuwa madhubuti na wenye umoja zaidi.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kuliunga mkono taifa la Palestina kwa njia zozote zile.

 

Akizungumzia utukufu wa Sikukuu ya Kubaathiwa Mtume (SAW), Ayatullah Khamenei amesema, Kubaathiwa na kupewa Utume Mtume Mtukufu ilikuwa ni zawadi yenye thamani kubwa ya Mwenyezi Mungu kwa jamii ya wanadamu.

Sanjari na kutoa mkono wa kheri na fanaka kwa Waislamu wote kote duniani kwa mnasaba huu adhimu, Kiongozi Muadhamu amesema ujumbe wa Mab'ath ya Mtume wa Allah (SAW) unamdhaminia mwanadamu Saada na mafanikio hapa duniani hadi Siku ya Kufufuliwa.

4122837

captcha