IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Jordan kwa wanawake yanaanza mjini Amman

22:19 - March 05, 2023
Habari ID: 3476663
TEHRAN (IQNA) - Mashindano ya 14 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Jordan kwa wanawake yalianza katika mji mkuu wa nchi hiyo , Amman Jumamosi jioni.

Wawakilishi kutoka nchi 50 wanashiriki katika hafla hiyo ya Qur'ani, akiwemo hafidha  kutoka  Iran Roya Fazaeli.

Kategoria pekee ya shindano hilo ni kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu, kulingana na tovuti ya Ad-Dostur.

Washindani wote kwanza hushiriki katika jaribio la awali ili kuamua kiwango chao cha kuhifadhi. Wale waliopata alama 85 kati ya 100 watafuzu raundi inayofuata.

Washiriki watano kati ya hao watatangazwa kuwa washindi bora mwishoni mwa shindano hilo. Washindi wa juu wanapaswa kuwa kati ya wale wanaopata angalau pointi 85.

Kabla ya kuondoka Tehran kuelekea Amman, Fazaeli aliiambia IQNA kuwa yuko tayari kushiriki mashindano hayo.

"Kwa kuzingatia kwamba hivi karibuni nimepitia mashindano mawili muhimu ya Qur'ani kwa mafanikio, kiwango hiki cha maandalizi kinaweza kunisaidia katika mashindano haya," alisema.

Fazaeli alishinda kitengo cha kuhifadhi Mashindano ya 45 ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran mwezi Januari. Huu ni uzoefu wake wa kwanza katika mashindano ya kimataifa.

Kutokana na kufanana kati ya kanuni za mashindano katika nchi za Kiarabu, wawakilishi wa mataifa haya wanaweza kuwa na nafasi kubwa zaidi ya kushinda, alisema, akiongeza kuwa hata hivyo, matokeo yanaweza pia kuwa "ya kushangaza".

Mashindano ya wanaume huko Jordan yatafanyika Aprili 11-17.  Ali Reza Sameri ataiwakilisha Iran katika kitengo cha kuhifadhi Qur'ani Tukufu nzima.

4125885

captcha