IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Mkakati wa sasa wa Ulimwengu wa Kiislamu uwe ni kuwaimarisha wapigania ukombozi ndani ya Palestina

22:11 - April 22, 2023
Habari ID: 3476902
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: mkakati wa sasa wa Ulimwengu wa Kiislamu inapasa uwe ni kuwasaidia na kuwaimarisha wapigania ukombozi ndani ya Palestina.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameyasema hayo leo alipohutubia mkutano wa hadhara wa wananchi, viongozi wa Mfumo wa Kiislamu na mabalozi wa nchi za Kiislamu walioko hapa nchini kwa mnasaba wa sikukuu ya Idul Fitr.

Ayatullah Khamenei ameutaja umoja kuwa ni hitajio la dharura na muhimu la Umma wa Kiislamu na akaashiria kuporomoka kunakohisika kwa utawala haramu wa Kizayuni na kupungua waziwazi nguvu zake za kuzuia hujuma, na akasema: maendeleo haya muhimu yametokea kwa baraka za Muqawama wa taifa na vijana wa Palestina, na stratejia ya sasa ya Ulimwengu wa Kiislamu inapasa ijikite katika kuwasaidia na kuwaimarisha wanaopambana ndani ya Palestina.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekumbusha kuwa suala la Palestina si la Kiislamu tu bali ni la kiutu pia na akaashiria mikusanyiko na maandamano ya Siku ya Quds yaliyofanyika katika nchi zisizo za Kiislamu na akasema: mikusanyiko ya kupinga Uzayuni ya Siku ya Quds ndani ya Marekani na katika nchi za Ulaya ni matokeo ya kuzidi kudhihirika kila leo jinai za Wazayuni maghasibu.

Ameongezea kwa kusema: kujitokeza watu wa Ulaya katika kuwaunga mkono wananchi wa Palestina, tena katika nchi tegemezi kwaWazayuni ni jambo muhimu sana.

Ayatullah Khamenei amesema, sababu kuu iliyoufanya utawala wa Kizayuni uwe katika hali mbaya mno ni mapambano yaliyobarikiwa ya wananchi yanayoendeshwa ndani ya Palestina, na moyo wa kujitolea wa kuhatarisha maisha na kujitoa mhanga vijana wa Kipalestina; na akasisitiza kwa kusema: hali ya sasa katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu inathibitisha kuwa, kadiri muqawama na kusimama imara wananchi wa Palestina katika maeneo mbalimbali kunavyozidi kuongezeka, ndivyo utawala bandia unavyozidi kuwa dhaifu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, kupambana kwa jina la Uislamu ndio sababu kuu ya kupata nguvu mapambano ya makundi ya Palestina; na akakumbusha kuwa, katika zama ambapo hakukuwa na mielekeo ya Kiislamu mafanikio haya hayakuwepo.

Aidha, Ayatullah Khamenei ameashiria jinsi Imam Khomeini (MA) na Jamhuri ya Kiislamu zilivyotangulia kuunga mkono suala la Palestina na akasisitiza kwa kusema: "harakati hii itaendelea; na tuna matumaini kuwa iko siku wananchi azizi wa Iran watakuja kushuhudia Waislamu wa nchi zote za Kiislamu wanasali Quds Tukufu kwa uhuru kabisa".

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria matatizo ya nchi za Kiislamu na akasema: kama amri ya Qur'ani ya "umoja wa kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu" itafanyiwa kazi, Ulimwengu wa Kiislamu wenye watu wapatao bilioni mbili na ulioko kwenye maeneo muhimu na nyeti zaidi za kijiografia duniani unaweza kupiga hatua za kutatua matatizo yaliyopo.

Ayatullah Khamenei ameashiria kuporomoka kidogokidogo utawala wa Kizayuni na akasema; "uporomokaji huu ambao ulianza miaka kadhaa nyuma umeshika kasi katika wakati huu; na Ulimwengu wa Kiislamu unapaswa kuitumia fursa hii adhimu".

4135968

captcha