IQNA

Ifahamu Qur'ani Tukufu/6

Nuru Isiyozimika Kamwe

22:44 - June 12, 2023
Habari ID: 3477138
TEHRAN (IQNA) – Taa zote zilizopo hapa duniani zitazimika siku moja. Hata jua halitaangaza tena siku ya kiama itakapokuja.

Lakini Mwenyezi Mungu anazungumza juu ya kitu katika Qur’ani Tukufu ambacho nuru yake haitazimika.

Katika tafsiri ya  Aya hii  174 ya Surati An-Nisa, watu wote wa dunia wanaambiwa; Enyi watu mlioamini Hakika imekujieni dalili zilizo wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na tumekuleteeni nuru iliyo wazi.

Kuna vishazi viwili muhimu katika  tafsiri aya hii; ushahidi dhahiri (Burhan kwa Kiarabu) na ‘mwanga ulio wazi’ (Nur Mubin kwa Kiarabu). Kwa mujibu wa Hadith, Burhan anarejelea kwa Mtume Mtukufu (s.a .w.w) na Nur Mubin anarejelea Qur’ani Tukufu.

Mtume Mtukufu  (s.a.w.w.) kwa hakika ni thibitisho kwa dini kwa sababu ameleta kitabu kama hicho bila ya kuhudhuria madarasa yoyote na kadiri muda unavyosonga mbele na sayansi ndivyo ndivyo ukweli wa mafundisho yake unavyozidi kuwa wazi zaidi.

Swali hapa ni kwamba nuru iko wazi yenyewe, basi kwa nini Qur’ani Tukufu inatajwa kuwa ni nuru iliyo wazi katika Tafsiri ya  aya hii?

Qur’ani ni nuru iliyo wazi na pia inatoa mwanga katika mambo mengine. Ni muongozo kwa wote na bila ya hayo watu hupoteza njia na hawawezi kufikia hatima yao.

Katika Tafsiri ya  aya hii na inayofuata, Mwenyezi  Mungu anafafanua nuru hii. Kutoka kwa Mola wako Mlezi kunaashiria ukweli kwamba nuru inatoka kwa Mwenyezi  Mungu na Yeye ndiye chanzo cha nuru hii.

Katika Tafsiri ya  Aya hii 175, Mwenyezi Mungu anasema; Wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na wakashikamana Naye, bila shaka atawaingiza kwenye rehema na fadhila zitokazo Kwake, na Atawaongoza Kwake kwenye Njia Iliyo Nyooka.

Hivyo basi, imani na kushikamana na nuru ya Qur'ani Tukufu kutapelekea mtu kunufaika na rehema ya Mwenyezi Mungu na kutengeneza njia ya mwongozo wake utakaomfikisha peponi na baraka zake za milele.

Kushikamana na nuru ya Qur’ani katika Tafsiri ya  aya hii ina maana ya kuzingatia mafundisho ya Kitabu kitukufu cha mwenyezi mungu na kuyafanyia kazi, ambayo humuongoza mtu kwenye Njia Iliyo Nyooka.

 

3483908

Kishikizo: nuru Qur'an tukufu
captcha