Tukio hilo lilitokea wakati mamia ya waumini walipokuwa wakisali Sala ya Ijumaa katika msikiti wa kati wa jiji hilo, msemaji wa Baraza la Imarati la Zaria Abdullahi Kwarbai alisema. "Miili minne ilipatikana awali, na kisha wengine watatu walipatikana baada ya timu ya uokoaji kupekua msikiti ulioporomoka," alisema.
Maafisa wa serikali walisema msikiti huo ulijengwa katika miaka ya 1830. Watu 23 walipelekwa hospitalini, Shirika la Usimamizi wa Dharura la serikali lilisema. Video zilizorekodiwa katika eneo la tukio zilionyesha mwanya mkubwa ambapo sehemu ya paa ilianguka. Gavana wa jimbo la Kaduna Uba Sani aliagiza uchunguzi wa haraka kuhusu maafa hayo ufanyike na akaahidi kuwasaidia walioathirika na "tukio hilo la kuhuzunisha".
Tukio hilo linafuatia zaidi ya majengo kumi kuporomoka katika taifa hilo la Afrika Magharibi katika mwaka uliopita pekee. Mara nyingi wenye mamlaka hulaumu majanga kama hayo kwa kushindwa kwa maofisa kutekeleza kanuni za usalama wa majengo na matengenezo duni na vifaa duni vya ujenzi.
4161890