Idara ya Masuala ya Kiislamu na Shughuli za Hisani huko Dubai imetangaza mradi kabambe wa Utalii wa Kiislam unaolenga kuimarisha utalii wa Kiislamu katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE)..
Msikiti huo, umepangwa kukamilika mnamo 2024 ambapo muundo wake unajumuisha ghorofa tatu, kila moja ikitumikia kwa lengo maalumu. Ghorofa ya kwanza ni eneo la sala , ghorofa ya pili ni ukumbi wa shughuli mbali mbali , na ghorofa ya tatu ina maonyesho ya Kiislamu. Msikito huo wa chini ya maji utakuwa na uwezo wa kuhudumia waumini kati ya 50 hadi 75 kwa wakati moja na mradi huu wa ajabu unaahidi kuleta mwanga wa utulivu wa kiroho na uboreshaji wa kitamaduni.
Zaidi ya hayo, msikiti huo utakuwa na maonyesho ya Qur'ani yanayoelezea safari ya Msahafu wa Sheikh Maktoum bin Rashid Al Maktoum tangu kuzinduliwa kwake hadi usambazaji wa nakala za Msahafu huo hivi karibuni duniani kote.
Mradi huo wa kihistoria ulitangazwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari siku ya Alhamisi na kuhudhuriwa na maafisa, akiwemo Dk Hamad Al Sheikh Ahmed Al Shaibani, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Masuala ya Kiislamu na Shughuli za Hisani huko Dubai, na watu wengine mashuhuri kutoka idara mbalimbali.
"Mradi wa Utalii wa Kidini huko Dubai" unalenga kukuza hadhi ya Dubai kama kitovu cha utalii wa kidini, kuwakaribisha wageni wa asili zote.
Dk Abdullah Ibrahim Abdul Jabbar, Mkuu wa Mpango wa Utalii wa Kidini, alisema kuwa mradi huo unajumuisha mfululizo wa mipango, ikiwa ni pamoja na Dubai Iftar, mkusanyiko wa kipekee wa wawakilishi wa kidini, na kutembelea misikiti ya kihistoria, mipya na mashuhuri. Pia inaangazia programu za kijamii, michezo na elimu ndani ya mpango wa "Halal Ramadhani", kukuza umoja na mabadilishano ya kitamaduni.
/3485270