IQNA

Kimbunga cha Al Aqsa

Maandamano ya kulaani jinai za Israel huko Gaza yaendelea duniani kote

10:21 - October 28, 2023
Habari ID: 3477799
TEHRAN (IQNA) Maelfu ya waandamanaji wameendelea kujitokeza mitaani kulaani hujuma ya Israel dhidi ya Ghaza na kuonyesha kuwaunga mkono Wapalestina.

Huko Mauritania wananchi waliandamana nje ya Ubalozi wa Marekani katika mji mkuu, Nouakchott siku ya Ijumaa huku Israel ikiendeleza vita vyake vya mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Ghaza.

Waandamanaji walisikika wakitoa nara wakiitaka Marekani kuwajibika kwa mashambulizi yanayoendelea ya Israel katika eneo lililozingirwa la Wapalestina.

Aidha mamia ya watu wa Tunisia waliandamana nje ya Ubalozi wa Ufaransa katika mji mkuu wa taifa hilo Tunis siku ya Ijumaa kulaani jinai za Israel dhidi ya Wapalestina. Maandamano kama hayo ya kulaania utawala haramu wa Israel yamefanyika siku za hivi karibuni katika nchi kadhaa za Afrika zikiwemo Afrika Kusini, Kenya, Nigeria na Morocco.

Waandamanaji walionyesha uungaji mkono wao usioyumba kwa  Wapalestina wa Ghaza, wakithibitisha wakisisitiza kuwa mapambano ndio njia pekee ya kurudisha haki ya kukomboa ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Israel.

Huko Sana'a, mji mkuu wa Yemen, waandamanaji walilaani vikali mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na Israel hivi sasa dhidi ya Wapalestina. Wasyria pia walikusanyika katika Kambi ya Jaramana kutoa sauti zao kwa Wapalestina. Nchini Lebanon wananchi waliingia mitaani pia kulaani Israel na kutangaza kufungamana na Wapalestina wanaodhulumiwa. Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, pia walikusanyika kuonyesha mshikamano na watu wa Ghaza.

Mijumuiko sawa ya aina hiyo ilifanyika katika nchi nyingine kadhaa siku ya Ijumaa, zikiwemo Uturuki, Jordan na Pakistan pamoja na maeneo mengine mengi ya dunia ambapo maelfu ya watu waliandamana kulaani ukatili wa utawala ghasibu wa Israel.

Israel ilianzisha vita dhidi ya Ghaza tarehe 7 Oktoba baada ya makundi ya muqawama wa Palestina kuanzisha Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa  kwa kutekeleza  mashambulizi ya kushtukiza katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu ili kukabiliana na jinai kali za utawala huo ghasibu dhidi ya wananchi wa Palestina. Mashambulizi ya Israel dhidi ya Ghaza yamelenga maeneo ya mikusanyiko, zikiwemo hospitali, shule, misikiti na makanisa, na kuwafanya zaidi ya watu milioni moja kuyahama makazi yao katika eneo hilo lenye watu wengi, ambalo lina watu zaidi ya milioni 2.

4178155

Habari zinazohusiana
captcha