IQNA

Historia

Mkutano wa kimataifa kuhusu Makaburi ya Baqi wazinduliwa Qom

16:43 - April 19, 2024
Habari ID: 3478700
IQNA - Mkutano wa kimataifa uliopewa jina la "Makaburi ya Baqi, Mahali Walimozikwa Maimamu na Masahaba" umefanyika katika mji mtakatifu wa Iran wa Qom siku ya Alhamisi.

Hujjatul Islam Seyed Abdol Fattah Navab, mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Masuala ya Hija na Ziyara na Ayatullah Mohsen Qomi, mkuu wa masuala ya kimataifa katika  Ofisi ya Kiongozi Muadhamu ni miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho.

Kituo cha Utafiti wa Hija na Ziyara kimeandaa mkutano huo kwa ushirikiano na taasisi na vituo vingine 30  kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuharibiwa kwa makaburi ya Baqi mjini Madina.

Vitabu kumi na tano vilivyoandikwa kuhusu makaburi ya Baqi na waliozikwa humo pia vilizinduliwa wakati wa sherehe za ufunguzi.

Mkutano huo umehudhuriwa na wanazuoni, wanafikra na watafiti wa vyuo vikuu na seminari kutoka katika ulimwengu wa Kiislamu.

Kwa mujibu wa waandaaji, makala 66 ziliwasilishwa katika sekretarieti ya mkutano huo.

Washiriki katika tukio la siku mbili la kitaaluma wamejadili mada kama vile masomo ya kisiasa na kijamii kuhusu Baqi, tafiti za kisasa kuhusu Baqi, masomo ya kihistoria na ustaarabu wa Baqi, na masomo ya kimataifa kuhusu Baqi.

Makaburi katika Jannatul Al-Baqi (Makaburi ya Baqi) yalibomolewa kabisa na Mawahabi wenye misimamo mikali mnamo tarehe 8 Shawwal katika mwaka wa 1345 AH (Aprili 21, 1925).

3487987

Habari zinazohusiana
Kishikizo: janatul baqi madina
captcha