Rais Mohammad Shein wa Zanzibar ametoa ujumbe kwa taifa kwa mnasaba wa kuanza Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo amewataka Wazanzibari wazidisha kusoma Qur’ani katika mwezi huu mtukufu.
2012 Jul 22 , 15:38
Mshauri wa masuala ya Qur'ani wa kitengo cha masuala ya utamaduni cha Shirika la Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu la Iran amesema ujumbe wa makarii na mahafidh 77 kutoka Misri ambao unajumuisha walimu wa kiraa na hifdhi ya Qur'ani Tukufu umewasili nchini Iran sambamba na kuanza mwezi wa Ramadhani.
2012 Jul 21 , 22:45
Mashindano ya Qur'ani Tukufu yamepangwa kufanyika kesho Jumapili Ramadhani Pili katika Medani ya Mwembe Chai katika mtaa wa Temeke mjini Dar es Salaam kwa mnasaba wa kuwadia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
2012 Jul 21 , 14:40
Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania kikishirikiana na Waislamu wa nchi hiyo kimepanga kuandaa mashindano kadhaa makubwa ya Qur'ani Tukufu yatakayowashirikisha Waislamu wote wa Kishia na Kisuni kwa mnasaba wa kuwadia mwezi mtukufu wa Ramadhani.
2012 Jul 21 , 14:39
Mbinu ya kisasa kabisa za kuhifadhi Qur’ani Tukufu imewasilishwa katika maonyesho ya 20 kimataifa ya Qur’ani Tukufu Tehran.
2012 Jul 20 , 11:23
Qur'ani Tukufu ambayo inasemekana kuwa iliandikwa kwa mkono wa Imam Ali (as) inaonyeshwa katika kibanda cha shirika la uchapishaji la Hizmet la nchini Uturuki katika maonyesho ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu yanayoendelea mjini Tehran.
2012 Jul 19 , 13:58
Vipindi vilivyosajiliwa awali vya duru ya pili ya mashindano ya kiraa ya Qur'ani Tukufu yaliyopewa jina la Zawadi ya Msomaji wa Jordan vitarushwa hewani kupitia televisheni ya taifa na Idhaa ya Qur'ani ya nchi hiyo.
2012 Jul 18 , 15:41
Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa chenye makao yake katika mji mtakatifu wa Qum nchini Iran kimetangaza mpango wa kuandaa Olimpiadi ya Kimataifa ya Qur’ani na Hadithi katika zaidi ya nchi 40 duniani.
2012 Jul 18 , 15:26
Kibanda maalumu cha kuwaarifisha watu na shakhisa mashuhuri waliosilimu na kuikubali dini tukufu ya Kiislamu duniani kimeanzishwa kwa mara ya kwanza katika Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani mjini Tehran.
2012 Jul 18 , 15:22
Nakala ya kwanza kabisa ya Qur'ani zenye hati ya braille kwa ajili ya walemavu wa macho imezinduliwa nchini Yemen.
2012 Jul 17 , 21:20
Jumuiya ya Reyhan-Der ya Uturuki imewatunuku watoto 700 nakala za Qur'ani Tukufu katika mji wa Merzifon katika mkoa wa Amasya kwa mnasaba wa kukaribia mwezi mtukufu wa Ramadhani.
2012 Jul 17 , 21:20
Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani yakiwemo ya wanachuo Waislamu ambayo huandaliwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huwa na nafasi muhimu katika kuakisi sura halisi ya nchi hii na viongozi wake.
2012 Jul 17 , 13:07
Balozi na mwambata wa kiutamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Falme za Kiarabu siku ya Alkhamisi ijayo wanatazamiwa kushiriki kwenye maonyesho ya sanaa mjini Doha Qatar ambapo msanii mashuhuri wa Iran anatazamiwa kuonyesha kazi zake za uandishi wa Qur'ani kwa kutumia mkono.
2012 Jul 17 , 12:44