Mashindano ya kimataifa ya 11 ya Qur'ani Tukufu yameanza huko Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu.
2012 Jul 28 , 18:59
Kitabu kinachozungumzia Ahlul Bait wa Mtume (saw) kwa lugha ya Kimalagasi kinaonyeshwa katika maonyesho ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu yanayoendelea mjini Tehran katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
2012 Jul 28 , 17:21
Shirika la SinarMas ambalo ni moja ya mashirika ya uzalishaji vyakula na mazao ya kilimo mjini Jakarta nchini Indonesia limesambaza mamia ya nakala za Qur'ani Tukufu miongoni mwa mayatima wa mji huo kama zawadi za mwezi mtukufu wa Ramadhani.
2012 Jul 25 , 15:42
Chuo cha kwanza cha Kutadabari Qur'ani na Hadithi na Utekelezaji Wake kimefunguliwa mjini Bani Suwayf nchini Misri na Swalah Sultan, mwanachama wa Muungano wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu.
2012 Jul 25 , 15:28
Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu wa Iran amepongeza Shirika la Kimataifa la Habari za Qur'ani IQNA kwa utendaji wake bora na kulitaja shirika hili kuwa ni rasilimali kubwa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
2012 Jul 24 , 17:53
Maonyesho ya nuskha za Qur'ani Tukufu zilizoandikwa kwa mkono katika karne za kale, yamepangwa kufanyika mjini Dubai tokea tarehe 27 mwezi huu wa Julai kwa ushirikiano wa Kituo cha Utamaduni na Turathi cha Imarati.
2012 Jul 24 , 17:52
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu ISESCO, limepanga kupongeza na kumshukuru Hasna Khulali, mshindi wa kwanza wa mashindano ya Qur'ani Tukufu yaliyofanyika hivi karibuni nchini malaysia.
2012 Jul 24 , 17:49
Ujumbe wa makari na mahafidh 77 kutoka nchini Misri ambao uko hapa nchini kwa mwaliko wa Idara ya Masuala ya Qur'ani Tukufu na Maarifa ya Kidini ya Taasisi ya Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu umetembelea taasisi ya Darul Qur'anil Karim.
2012 Jul 24 , 17:11
Hafla ya Kufarijika na Qur'ani' ambayo imewajumuisha makari na mahafidh wa Qur'ani Tukufu wapatao 77 kutoka nchini Misri imefanyika leo mchana katika Taasisi ya Mawasiliano ya Kiislamu ya Iran mjini Tehran.
2012 Jul 23 , 17:43
Hafla ya kuhitimisha Qur'ani Tukufu na usomaji wa mashairi ya Kiislamu ilifanyika siku ya Jumamosi katika Msikiti wa Zeinabiyya (as) katika mji wa Istanbul nchini Uturuki.
2012 Jul 23 , 17:40
Kitengo cha 'Utamaduni na Mataifa ya Waislamu' katika Maonyesho ya 20 ya Kimataifa ya Qur'ani kimezinduliwa katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini RA mjini Tehran.
2012 Jul 22 , 15:44
Sambamba na siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, mwezi ambao Qur'ani Tukufu iliteremshwa dnani yake, alasiri ya jana Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alishiriki katika najlisi ya kiraa ya Qur'ani iliyoshirikisha makarii na mahafidhi wa kitabu hicho kitukufu.
2012 Jul 22 , 15:38
Rais Mohammad Shein wa Zanzibar ametoa ujumbe kwa taifa kwa mnasaba wa kuanza Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo amewataka Wazanzibari wazidisha kusoma Qur’ani katika mwezi huu mtukufu.
2012 Jul 22 , 15:38