IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Msingi imara wa uungaji mkono wa wananchi ni hoja kamili kwa wote

21:44 - February 23, 2023
Habari ID: 3476615
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo Alkhamisi ameonana na wajumbe wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu wanaomchagua na kusimamia kazi za Kiongozi Muadhamu wa Iran na kusisitiza kuwa, msingi madhubuti na imara wa uungaji mkono wa wananchi kwa Jamhuri ya Kiislamu ni hoja kamili kwa viongozi na maulamaa wote.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo na kuongeza kuwa, Baraza la Wanazuoni Wataalamu ni muhimu sana na ni nembo ya mshikamano baina ya Jamhuri na Uislamu, vitu viwili vikuu vinavyounda mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 

Amesema, msingi imara wa uungaji mkono wa wananchi kwa mfumo huo wa Kiislamu ni utajiri wa taifa ambao Mwenyezi Mungu amekamilisha hoja Zake kwa maulamaa na viongozi wote wa mfumo huo, hivyo kila mtu anapaswa kufanya juhudi zisizochoka za kuilinda na kuongeza uwekezaji katika hazina hiyo adhimu.

Vile vile amesema, hadhi, nafasi na umuhimu mkubwa wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu ni mkubwa zaidi kuliko taasisi nyingine yoyote ya mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na kuongeza kuwa, baraza hilo ndilo linalomchagua Kiongozi Muadhamu na ndilo linalosimamia kazi zake na ndilo linaloamua kuwepo na kuendelea mazingira ya Kiongozi Muadhamu, na hiyo ni nafasi adhimu na jukumu zito linalobebwa na wajumbe wa baraza hilo. 

Amesema, kulifanyia uadui Baraza la Wanazuoni Wataalamu ni kuufanyia uadui mfumo mzima wa Jamhuri ya Kiislamu na kuongeza kuwa, baadhi ya uadui inaofanyiwa Jamhuri ya Kiislamu unahusiana na masuala ya kisiasa na misimamo yake kuhusu baadhi ya mambo kama kadhia ya Palestina, lakini baadhi ya uadui unahusu dhati na mfumo wenyewe wa Jamhuri ya Kiislamu.

Mwanzoni mwa kikao hicho, Sayyid Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye pia ni Naibu wa Mkuu wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu amewasilisha ripoti fupi kuhusu kazi za baraza hilo.

4123950

captcha