IQNA

Mawaidha

Tofauti kati ya Muislamu na Muumini

19:58 - January 14, 2024
Habari ID: 3478197
IQNA-Kimsingi, kila anayetamka Shahada mbili anahesabiwa kuwa mfuasi wa Uislamu na hukmu za Uislamu zinamhusu yeye.

Imani, hata hivyo, imani ni ile itikadi ya kweli ndani ya moyo sio tu kidhahiri na kwa ulimi. Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 14 ya Surah Al-Hujurat:

Mabedui wamesema: Tumeamini. Sema: Hamjaamini, lakini semeni: Tumesilimu. Kwani Imani haijaingia katika nyoyo zenu. Na mkimt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hatakupunguzieni chochote katika vitendo vyenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.”

Mtu anaweza kuwa na misukumo tofauti ya kuwa Mwislamu, ikijumuisha motisha za kifedha, kifamilia na masilahi ya kibinafsi.­­­­ Lakini Iman imejikita katika Ilm (elimu) na misukumo ya kiroho.

Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) amesema kuwa Muislamu ni suala linaloonekana kidhahiri lakini nafasi ya Imani ya kweli  iko moyoni.

Pia, kwa mujibu wa Hadith nyingine, kuwa Muislamu kunahisika na kutamka Shahad mbili tu, lakini Iman pia au kuwa Muislamu wa kweli kunajumuisha vitendo au kutekeleza maamurisho ya Uislamu..

Imani ni sehemu ya Uislamu na kwa msingi huo kila muumini ni Muislamu lakini si kila Muislamu ni Muumini.

3486798

Kishikizo: imani muislamu hujurat
captcha