IQNA

Jinai za Israel

UN: Watu Milioni 2 huko Gaza wanapata matatizo makubwa ya kimaisha kila siku

17:57 - April 17, 2024
Habari ID: 3478694
IQNA - Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu hali mbaya katika Ukanda wa Gaza ambapo watu wanahangaika maisha kila siku, ukitangaza kuwa utazindua ombi la kimataifa la dola bilioni 2.8 kwa Gaza na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.

Watu milioni 2 ambao hadi sasa wamenusurika mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza wanatatizika maisha kila siku, mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) katika eneo linalokaliwa la Palestina, Andrea De Domenico, aliwaambia waandishi wa habari Jumanne.

De Domenico alisema ombi la kimataifa la misaada limezinduliwa Jumatano.

Amesema ombi hilo ni la "kuunga mkono watu milioni 3 waliotambuliwa kote Ukingo wa Magharibi na Gaza."

Alisema asilimia 90 ya misaada hiyo itaenda Gaza na ofisi yake ilipanga awali kuomba dola bilioni 4 lakini ikapunguza idadi hiyo kutokana na uwezo mdogo wa kusambaza misaada.

Akibainisha kuwa njaa inatokana na kukosekana kwa chakula, usafi, maji na vituo vya afya, de Domenico alisema, "kutokuwa na uhakika ni ukweli wa kila siku kwa watu wa Gaza."

Alisema kuwa familia zinazokuja kusini mwa Gaza zimefurushwa mara saba, na siku mbili zilizopita timu yake iliona maelfu wakipanga foleni kuelekea kaskazini.

Israel ilianzisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza Oktoba 7 baada ya operesheni ya kulipiza kisasi ya wapigania ukombozi wa Palestina na hadi sasa jeshi katili la Israel limeua takriban Wapalestina 33,800, wengi wao wakiwa wanawake na watoto na wengine 76,500 kujeruhiwa huku kukiwa na uharibifu mkubwa na uhaba wa mahitaji.

3487972

Habari zinazohusiana
captcha