Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Waislamu Ethiopia huukaribishwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa raghba kubwa ya kidini. Imekuwa ni jambo la kawaida kwa Waislamu kujaa katika misikiti na kupelekea barabara za kando kufungwa ili Waislamu waweze kupata nafasi ya kusimamisha ibada.
“Ethiopia ina nafasi muhimu kama nchi yenye wafuasi wa Uslamu, Ukristo na Uyahudi,” amesema Profesa Mohammed Zekeriya katika mahojiano na Shirika la Habari la Anadolu. Zekeriya ni mshauri maalumu wa Taasisi ya Utafiti wa Ethiopia katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa.
“Ethiopia imetajwa katika vitabu vya Kiislamu kama eneo la kukimbilia na kupata hifadhi,” amesema. “Mtu wa kwanza aliyetamka takbir ya kwanza katika mji mtakatifu wa Makka alikuwa, Bilal, Muethiopia.
Zekeriya amesema hiyo ni nukta inayoashiria uhusiano wa jadi baina ya watu wa Ethiopia na Bara Arabu.
“Mfalme wa Ethiopia alikuwa mkarimukwa wakimbizi wa kwanza Waislamu waliofika Abyssinia (Ethiopia) kwa amri ya Mtume Muhammad SAW,” amesema.
Waislamu wanakadiriwa kuwa takriabani asilimia 40 ya idadi ya watu milioni 94 nchini Ethiopia.../mh