IQNA

Ongezeko la asilimia 91 la chuki dhidi ya Waislamu Marekani

18:39 - July 18, 2017
Habari ID: 3471074
TEHRAN (IQNA)-Kumeshuhudiwa ongezeko kubwa la chuki dhidi ya Waislamu Marekani kutokana na rais Donald Trump wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa Jumatatu na Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR), kumeripotiwa visa 940 vya chuki dhidi ya Waislamu Marekani kuanzia Aprili hadi Juni mwaka huu.

CAIR imesema hilo ni ongezeko la asilimia 91 ikilinganishwa na kipindi sawa na hicho mwaka 2016. Halikdhalika ripoti hiyo imesema kati ya vitendo hivyo vya chuki dhidi ya Waislamu asilimia 12 ilijumuisha kubugudhiwa na Idara ya Upelelezi FBI.

Halikadhalika asilimia 33 ya vitendo hivyo vya hujuma vilijumuisha kushambuliwa misikiti au maeneo ya ibada.

Ingawa katika ripoti yake CAIR haikumtaja moja kwa moja Donald Trump kuwa chanzo cha chuki dhidi ya Uislamu, lakini utafiti uliofwanya na Chuo Kikuu cha California ulibaini kuwa kumekuwpeo na ongezeko la hujuma dhidi ya jamii za waliowachache tangu Trump atangazwe mshindi katika uchaguzi wa rais mwezi Novemba mwaka jana.

Wataalamu wanasisitiza kuwa, matamshi ya kibaguzi ya Trump pamoja na sera zake hasa za kuwapiga marufuku Waislamu kutoka nchi sita kuingia Marekani  ni chanzo cha chuki, mashambulizi na hujuma zinazofanywa na makundi ya kibaguzi dhidi ya Waislamu katika miji mbalimbali nchini humo.

3463388

captcha