IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Ethiopia yamalizika, Mmorocco aibuka wa kwanza

17:07 - June 14, 2022
Habari ID: 3475375
TEHRAN (IQNA) - Mshiriki kutoka Morocco ametwaa tuzo ya juu katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Ethiopia.

Ilias El Mehyaoui, kijana wa Morocco siku ya Jumatatu alishinda nafasi ya kwanza ya Mashindano ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Zaidi ya washindani 50 kutoka nchi tofauti za Kiislamu walishiriki katika mashindano hayo.

“Namshukuru Mungu kwa ushindi huu. Kutawazwa huku si jambo la kushangaza kwa Wamorocco ambao wamezoea kung'ara na kujipambanua katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani," Ilias El Mehyaoui katika mazungumzo na wanahabari.

El Mehyaoui alisema ni heshima na taadhima kwake kushinda nafasi ya kwanza, na kuongeza, "Natoa ushindi huu kwa Mfalme Mohammed VI na watu wa Morocco. Pia nautunuku ushindi huu kwa familia yangu, wazazi na masheikh walionifundisha.”

Washiriki wengine kutoka Jordan na Lebanon walishinda katika kategoria za usomaji na Adhan  mtawalia.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Ethiopia FBC, moja ya mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani ni kukuza nafasi maalum ya Ethiopia katika dini ya Kiislamu kama ardhi ya kwanza iliyokuwa kimbilio la kwanza nje ya Makka kwa masahaba wa Mtume Muhammad (SAW).

Mzaliwa huyo wa mji wa Oujda kaskazini-mashariki mwa Morocco, awali alishinda nafasi ya tatu katika kitengo cha qiraa ya Qur'ani katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Malaysia mwaka 2019.

Wasomaji kadhaa wa Qur'ani wa Morocco katika miaka iliyopita wameonyesha utendaji bora katika mashindano mashuhuri duniani kote.

Mwezi uliopita, Mohamed Qastali alishinda tuzo ya pili katika toleo la tano la Mashindano ya Kuhifadhi Qur'ani ya Katara nchini Qatar, na kuwashinda washiriki zaidi ya 900 kutoka nchi 48, zikiwemo nchi 32 zisizo za Kiarabu.

3479294

captcha