IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Iran

Finali za Mashindano ya 39 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran kufanyika Februari

12:06 - December 22, 2022
Habari ID: 3476285
TEHRAN (IQNA)- Finali za Mashindano ya 38 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu Iran zitaanza katika mji mkuu wa Iran, Tehran, mnamo Februari 18, 2023.

Hayo yamedokezwa na Hamid Majidimehr, Mkuu wa Qur'ani na Naibu wa Etrat katika Shirika la Masuala ya Wakfu na Misaada Iran ambapo  katika mahojiano na IQNA amesema kwamba nchi 80 zimewatambulisha wawakilishi wao kwenye mashindano hayo.

Amesema nchi zilizoshiriki katika mashindano yaliyopita ni 68 na kuongeza kuwa, kuongezeka kwa idadi ya nchi mwaka huu kunaonyesha juhudi za Iran zilizozaa matunda katika uga wa diplomasia ya Qur'ani Tukufu.

Kauli mbiu ya mashindano ya 38 itakuwa sawa na ya mashindano yaliyopita ambayo, ni "Kitabu Kimoja, Umma Mmoja", jambo ambalo linaashiria namna Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inavyosisitiza kuhusu umoja na udugu kati ya mataifa ya Kiislamu, alisema.

Kwa mujibu wa afisa huyo, hatua ya awali ya mashindano hayo itafanyika kwa njia ya kutohudhuria washiriki Januari 13-14, ambapo wajumbe wa jopo la majaji watakusanyika katika mji mtakatifu wa Mashhad ulio kaskazini mashariki mwa Iran kwa ajili kutazama na kutathmini klipu zilizotumwa za washindani na kuchagua wale ambao wanaweza kufuzu kwa fainali.

Kutakuwa na wataalamu 12 wa Qur'ani Tukufu watakaohudumu katika jopo la majaji katika kitengo cha wanaume na wataalamu 12 wanaohudumu katika kitengo cha wanawake, alibainisha.

Faili zilizorekodiwa zimepokelewa na kamati ya maandalizi kutokana na ushirikiano wa balozi za Iran na vituo vya kitamaduni vya Iran kote duniani na pia kwa ushirikiano wa  Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa na taasisi za Qur'ani, Majidimehr alisema.

Wale watakaofika hatua ya fainali wataanza kushindana katika fainali Februari 13, sambamba na Siku ya Maba’ath (kuashiria kuteuliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) kama mjumbe wa mwisho wa Mwenyezi Mungu), aliongeza.

Shirika la Masuala ya Wakfu na Misaada Iran kila mwaka huandaa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani kwa kushirikisha wanaharakati wa Qur'ani kutoka nchi mbalimbali.

Toleo la 38, lilifanyika mnamo Machi 2022 kwa sababu ya wasiwasi juu ya janga la coronavirus.

4108692

captcha