IQNA

Jinai za Marekani

Al Sudani: Marekani ilikiuka mamlaka ya kujitawala Iraq kwa kuwaua Jenerali Soleimani na Al Muhandis

12:51 - January 06, 2023
Habari ID: 3476365
TEHRAN (IQNA)- Waziri Mkuu wa Iraq, Mohammed Shia' al-Sudani amemuenzi kamanda wa ngazi ya juu wa kupambana na ugaidi wa Iran, Luteni Jenerali Qassem Soleimani na mwenzake wa Iraq, Abu Mahdi al-Muhandis, waliouawa katika shambulio la kigaidi la ndege zisizo na rubani za Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad miaka mitatu iliyopita, na kusema kuwa mauaji hayi yalikuwa "shambulio kali" dhidi ya uhuru na mamlaka ya kujitawala Iraq.

“Uhalifu wa kuwaua ‘Makamanda wa Ushindi’ na wanajihadi wenzao ulikuwa ni ukiukaji wa wazi wa wa mamlaka ya kitaifa ya Iraq. Mauaji ya kuratibiwa dhidi ya makamanda, ambao walikuwa na jukumu kubwa katika kutokomeza janga la ugaidi, ni kutoheshimu kabisa makubaliano ya pande mbili [yaliyotiwa saini kati ya Baghdad na Washington]," Sudani alisema katika hafla ya Alhamisi katika mji mkuu wa Baghdad katika kumbukumbu ya makamanda wawili wa hadithi.

"Tuliamka Januari 3, 2020 kusikia habari mbaya kuhusu mauaji ya Abu Mahdi al-Muhandis, kamanda wa pili wa Jeshi la Kujitolea la Wananchi (PMU), na Jenerali Qassem Soleimani, ambaye alikuwa katika ziara rasmi nchini Iraq,” aliongeza.

Waziri Mkuu wa Iraq aliendelea kuushutumu utawala wa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kutokana na hatua yake ya kuamuru shambulio hilo la kinyama dhidi ya mamlaka ya kujitawala Iraq.

Al Sudani amesema mapambano dhidi ya ugaidi yanahitaji nguvu na ujasiri, na hii ilikuja kupitia roho ya kitaifa ya Wairaqi wote na fatwa iliyotolewa na kiongozi mkuu wa  kidini wa Iraq Ayatullah Ali al-Sistani.

Amesisitiza kuwa serikali yake inajitahidi kujenga msingi imara wa mamlaka ya Iraq, inajitegemea katika kufanya maamuzi, inajenga uhusiano kwa misingi ya maslahi ya pamoja, inalinda mipaka ya nchi, na itachukua hatua kukabiliana na hujuma yoyote dhidi ya Iraq na wageni wake.

Lt. Jenerali Soleimani, ambaye alikuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Naibu Kamanda Jeshi la Kujitolea la Wannachi wa Iraq (PMU) Abu Mahdi al-Muhandis, na wanamapambano wenzao waliuawa katika shambulio la ndege zisizo na rubani za Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad mapema  Januari 3, 2020. Shahidi Soleimani alikuwa ameelekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa serikali ya nchi hiyo.

Ikulu ya White House na Pentagon ilitangaza kuwa ilihusika na mauaji hayo ya kigaidi  na kuthibitisha kuwa shambulio hilo lilitekelezwa kwa maelekezo ya Rais wa Marekani wa wakati huo Donald Trump.

4112389

captcha