Mashuhuda waliripoti kuwa wanajeshi wa utawala dhalimu wa Israel walifyatua risasi za chuma zilizofunikwa kwa plastiki, mabomu ya machozi yenye sumu, na kutumia mizinga ya maji kuwashambulia waumini hao, wakiwafuata na kuwashambulia kimwili baadhi yao katika vurugu hizo.
Ni wachache tu waliofanikiwa kufika katika Msikiti wa Al-Aqsa kuswali Sala ya Ijumaa, kwani utawala ghasibu na wa kikoloni wa Israel ulitumia askari wake katili kuwazuia waumini kuingia katika eneo hilo takatifu.
Hii ni Ijumaa ya tatu mfululizo ambapo waumini wamekataliwa kuingia katika eneo la Msikiti wa Al-Aqsa. Kizuizi hiki kinachoendelea kimewalazimu kutekeleza sala zao katika mitaa ya jirani ya Wadi Al-Joz, ambayo ni karibu na Jiji la Kale la Quds Tukufu ambapo msikiti huo uko.
/3485756