IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Kwanza ya Qur'ani ya Kimataifa ya Kazakhstan yanaanza mjini Astana

17:17 - November 01, 2023
Habari ID: 3477824
ASTANA (IQNA) - Toleo la kwanza la Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu nchini Kazakhstan limeanza leo Jumatano asubuhi  katika mji mkuu, Astana.

Idara ya Kidini ya Waislamu wa Kazakhstan inaandaa mashindano hayo jijini Astana ambayo yanafanyika kwa muda wa siku mbili 2, 2023, ili kusherehekea Siku ya Jamhuri, ambayo ni sikukuu ya kitaifa.

Mashindano hayo ya kimataifa yatashirikisha washiriki 30 kutoka nchi tofauti, zikiwemo Indonesia, Malaysia, Iran, UAE, Saudi Arabia, Marekani, Misri, Uturuki, Russia, Kuwait na Guinea.

Washiriki watashindana katika kategoria ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu. Mashindano hayo yanafanyika katika Msikiti Mkuu wa Astana, msikiti mkubwa zaidi nchini Kazakhstan na Asia ya Kati.

Majaji ni wataalamu wa Qur'ani kutoka Uturuki, Misri, UAE, Saudi Arabia na Kazakhstan.

Mashindano hayo ya siku mbili ya Qur'ani yanaonyeshwa moja kwa moja kwenye majukwaa mbalimbali. Watazamaji wanaweza kuitazama kwenye chaneli ya TV ya Muftiyat "Munara TV" na kanali yake ya YouTube, au kwenye kurasa rasmi za mitandao ya kijamii za Idara ya Kidini ya Waislamu wa Kazakhstan.

Kazakhstan 1st Int’l Quran Competition

4179133

captcha