IQNA

Mashindano ya Qur'ani Tukufu

Wawakilishi wa Iran kwenye Mashindano ya Qur'ani mtandaoni la Iraqi apata zawadi

20:49 - November 04, 2023
Habari ID: 3477839
TEHRAN (IQNA) – Wawakilishi wa Iran wamechukua nafasi kadhaa za juu katika mashindano ya mtandaoni ya Qur’ani Tukufu yaliyoandaliwa na Iraq. Mashindano hayo yalipewa anuani ya "Walshafi Walwitr" ( Na kwa viwili viwili na kimoja kimoja) ambayo inarejelea aya ya 3 ya Surah Al-Fajr.

Hafla hiyo iliandaliwa kwa wanawake pekee mtandaoni na wafuasi wa Qari Sayyid Hassanayn Al-Halw wa Iraq katika kategoria tatu. Mashindano hayo yalimalizika Jumatano usiku.
Katika  kategoria ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu, iliyoshuhudia wahifadhi 83 wakishindana, Hananeh Khalafi kutoka Iran alishinda nafasi ya kwanza. Sareh Rahim Jabbar wa Iraq alishika nafasi ya pili akifuatiwa  Fatemeh Sadat Ghaffari wa Iran.
Jumla ya washiriki 68 walishiriki katika kategoria ya usomaji wa tarteel. Ozra Sabrinejad kutoka Iran alitwaa taji hilo huku Ahlam Naema Sharif na Fatima Khalid Kazem, wote kutoka Iraq wakishinda safu mbili zilizofuata.
Kategoria ya qiraa ilikuwa na  washiriki 43. Atefeh Naseh, Zahra Hosseinpur, na Ameneh Al-Bukhafnar, wote kutoka Iran, walichukua nafasi tatu za juu.
Jopo la majaji liliundwa na wataalamu kutoka Iran, Lebanon na Iraq.

4179482

captcha