IQNA

Mashindano ya Qur;ani

Washindi wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Dubai wazawadiwa

11:48 - March 24, 2024
Habari ID: 3478565
IQNA - Sherehe za kufunga toleo la 27 la Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Dubai ambayo hujulikana rasmi kama Tuzo la Kimataifa la Qur'ani Tukufu la Dubai (DIHQA) zilifanyika katika mji wa UAE Jumamosi jioni.

Washindi wa safu za juu katika shindano hilo walitajwa na kutunukiwa katika hafla hiyo iliyofanyika katika Jumuiya ya Utamaduni na Sayansi.

Mohammed Al Ammri kutoka Bahrain alichukua nafasi, kulingana na jopo la majaji.

Naji bin Sliman kutoka Libya alikuwa mshindi wa pili, huku Sheikh Tijan Ambi kutoka Gambia akishika nafasi ya tatu.

Katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Dubai Sheikh Mansoor bin Mohammed bin Rashid Al Maktoum pia alimtunuku Sheikha Hind bint Maktoum bin Juma Al Maktoum kwa tuzo ya Shakhsia wa Kiislamu wa Mwaka.

Tuzo hiyo ilitolewa kwa kutambua juhudi na mchango wake katika kuunga mkono harakati za Kiislamu, kibinadamu, hisani na kijamii.

Mashindano hayo huandaliwa kila mwaka katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

3487704

Habari zinazohusiana
captcha