Mashindano ya hifdhi ya Qur’ani Tukufu yamepangwa kufanyika kote Britani na Ireland ya Kusini mwezi baadaye mwaka huu.
2012 Aug 27 , 00:13
Mahafidhi wa Qur’ani Tukufu wa Palestina walioshiriki katika mashindano ya kimataifa katika nchi mbalimbali na kushika nafasi za juu wameenziwa katika sherehe iliyofanyika mjini Ramallah huko Palestina.
2012 Aug 27 , 00:13
Nakala ya kale ya Qur’ani Tukufu iliyoandikwa kwa hati za mkono mwaka 1237 Hijria na kutarjumiwa kwa lugha ya Kifarsi inaonyeshwa katika maaonyesho ya jimbo la Kashmir huko India.
2012 Aug 25 , 15:30
Karii mashuhuri wa Qur'ani wa Iran Hussain Yazdanpanah ameshinda mashindano ya Qur'ani ya Inna Lilmuttaqina Mafaza yaliyosimamiwa na televisheni ya Iran ya al Kauthar.
2012 Aug 21 , 18:21
Usiku wa 29 wa mashindano ya Qur'ani yanayoendeshwa na televisheni ya al Kauthar ya Iran ambayo yamepewa jina la "Inna Lilmuttaqina Mafaza" umeshuhudia mchuano mkali kati ya makarii wa Afghanistan na Qatar.
2012 Aug 18 , 18:50
Sherehe ya kuenzi na kuwashukuru washindi wa duru ya tisa ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu ilifanyika jana Jumanne katika msikiti mkuu wa mjini Algiers ikihudhuriwa na Rais Abdul Aziz Bouteflika wa nchi hiyo.
2012 Aug 15 , 18:40
Chama cha Uhuru na Uadilifu cha Harakati ya Ikhwanul Muslimin nchini Misri kimewataka mamilioni ya wananchi kuhudhuria katika Medani ya Tahrir mjini Cairo hapo kesho kwa ajili ya kuhitimisha Qur'ani Tukufu.
2012 Aug 15 , 16:03
Maonyesho ya nakala za kale zilizoandikwa kwa hati za mkono za Qur'ani Tukufu yanafanyika katika Akademia ya Sanaa, Utamaduni na Lugha Mbalimbali katika mji wa Srinagar kwenye jimbo la Jamu na Kashmin.
2012 Aug 14 , 18:37
Mbunge mmoja wa Misri ametoa wito wa kusitishwa uchapishaji wa nakala za Qur'ani Tukufu katika viwanda vya uchapishaji ambavyo havisimamiwi ipasavyo.
2012 Aug 14 , 18:36
Kitengo cha Utamaduni cha Haram ya Abulfadhil Abbas (as) katika mji mtakatifu wa Karbala nchini Iraq kimeadaa mahafali ya kila siku ya usomaji Qur'ani katika haramu hiyo kutokana na idadi kubwa ya wafanyaziara wa Kiirani wanaozuru haram hiyo na ile iliyo karibu ya Imam Hussein (as).
2012 Aug 14 , 13:39
Sherehe ya kuhitimisha Qur'ani Tukufu ilifanyika jana usiku huko Morocco na kuhudhuriwa na malaki ya watu.
2012 Aug 14 , 13:34
Maonyesho ya kwanza ya mabango ya kaligrafia ya aya za Qur'ani Tukufu yanaendelea kufanyika mkoani Taiz nchini Yemen. Maonyesho hayo yameandaliwa na taasisi ya Nyumba ya Sanaa ya nchi hiyo.
2012 Aug 13 , 16:06
Katika haditi zake nyingi Imam Ja'far Swadiq (as) amekutambua kuwa mbali na Qur'ani Tukufu na Suna za Mtume (saw) kuwa ndiyo sababu kuu ya mifarakano na hitilafu zilizopo kati ya Waislamu na aliona kwamba iwapo Waislamu watarejea katika Qur'ani na Suna basi hitilafu na migawanyiko yao itapungua sana.
2012 Aug 13 , 11:14