IQNA

Msimu wa Umrah kwa wasafiri wa kigeni Saudia kumalizika mwisho wa Shawwal

20:05 - April 27, 2022
Habari ID: 3475177
TEHRAN (IQNA)- Msimu wa sasa wa Hija ndogo ya Umrah kwa Waislamu kutoka nje ya Saudia utamalizika katika siku ya mwisho ya Mwezi wa Shawwal ambayo inatarajiwa kusadifina na Mei 31.

Wakuu wa Saudia wametoa tangazo hilo huku wakianza mpango wa kuwapokea Mahujaji kutoka nje ya nchi ambapo ibada ya Hija inatazamiwa kufanyika kwa mara ya kwanza baada ya miaka miwili.

Wizara ya Mambo ya Hija na Umrah ya Saudia imesema 30 Shawwal itakuwa siku ya mwisho kwa wasafiri kutoka nje ya nchi kutekeleza Hija ndogo ya Umrah.

Saudia imetangaza kuwa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani imetoa visa karibu milioni moja kwa ajili ya Waislamu kutoka nje ya ufalme kwa ajili ya Umrah. Kwa kawaida Mwezi Mtukufu wa Ramadhani huwa kilele cha msimu wa Umrah.

Saudia imeondoa vizingiti vingi ambavyo ilikuwa imeweka katika kipindi cha miaka mwili kuzuia kuenea ugonjwa wa corona nchini humo.

Hivi karibuni Mamlaka ya Saudia ilitangaza kwamba nchi hiyo itawaruhusu Waislamu milioni moja kushiriki katika ibada inayokuja ya Hija.

Wale wanaotoka nje ya Saudi Arabia watahitajika kuwasilisha matokeo hasi ya Covid-19 PCR kutokana na kipimo kilichochukuliwa ndani ya saa 72 kabla ya kusafiri.

3478684

Kishikizo: hija waislamu umrah saudia
captcha